Dunia na mambo yake yote yanapita!

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,600
19,502
Jaribu kutafakari hapo ulipo, tangu umezaliwa, umepata akili, watu wangapi uliowaona wanapambania maisha ya dunia hii, wako wapo, yale waliyopambania yamewasaidia nini kwa maisha yao huko walikoenda?

Wanaweza kuwa wamekula bata, wamelala na wanawake wawatakao au wanaume wawatakao, wamejenga nyumba wazitakazo, wamepata hela wazitakazo, vyeo wavitakavyo, wameonea watu vya kutosha, wamepata sifa za kutosha, wamedhulumu vya kutosha, wameiba pesa za uma vya kutosha, mwisho wa siku wameviacha, je? huko walikoenda wameenda mahali gani?

ni masikini wangapi umewaona na haujawasaidia, wagonjwa wangapi umewaona haujawasaidia, wenye njaa wangapi hujawapa chakula, waliokosa ada shule wangapi umeishia tu kuwacheka na kusema hawana bidii kutafuta pesa ni ombaomba, maisha yanapita, huko utakakoenda, umeandaaje maisha yako?

Eeeh Bwana nisaidie, utakapomiliki juu Eeh Bwana unikumbuke!

Hilo ndio ombi langu kila siku, Yesu utakaporudi naomba unikumbuke makaoni mwako. Kama nikifa kabla hujarudi basi nipe kibali nikapumzike kifuani pa Ibrahim🙏
 
Hilo ndio ombi langu kila siku, Yesu utakaporudi naomba unikumbuke makaoni mwako. Kama nikifa kabla hujarudi basi nipe kibali nikapumzike kifuani pa Ibrahim🙏
Mungu akubariki, Mungu akusaidie na akupe haja ya moyo wako kwa Jina la Yesu Kristo. kama kuna kitu kila mtu anatakiwa kuwaza ni where you will spend your eternity? aidha dunia ikiisha sasaivi, au ukifa kabla haijaisha, utaelekea wapi? maisha ya duniani ni mafupi, yajayo ni ya milele. ni ujinga mkubwa kwa mwanadamu kusumbukia yale ya muda mfupi kuliko yale ya milele. Glory and Honor to the Lamb of God!
 
Mwisho wa haya maisha ni bure hakuna atakayeondoka na fedha,mali,uzuri,cheo ushawishi nk vyote vitabaki duniani na kama vitabaki huku unakoenda utapeleka nini?ni zawadi gani tutampa bwana kutoka kwenye haya maisha?Ni vyema kuomba kifo kitukute vyema na tukiwa tumejiandaa.
 
hata huyo mama yao wanaomtaja mara nyingi kwa siku kuliko wanavyomtaja Mungu naye ataondoka tu tena bila chochote kabisa
 
Back
Top Bottom