Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,508
- 8,128
Kweli vidole havifanani, Dubai jana imetangaza ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wenye thamani ya Tshs trilioni 91 kusini mwa mji ambao utaambatana na ujenzi wa mji mpya(wilaya) ambao umeshaanza kujengwa wenye kilomita za mraba 145.
Gharama hizi za ujenzi ni zaidi ya mara mbili ya bajeti ya Tanzania ya mwaka jana Inayoishia June mwaka huu huku tukiwa na rekodi ya kushindwa kutimiza bajeti tunazoandaa wenyewe mara kwa mara kutokana na ukusanyaji duni wa mapato na pesa za wafadhili.
"Tunajenga mradi mpya kwa ajili ya vizazi vijavyo kuhakikisha maendeleo imara kwa ajili ya watoto wetu na watoto wao. Dubai itakuwa uwanja wa ndege wa dunia, bandari yake, mji na kituo kipya cha dunia" Amesema Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, mfalme wa Dubai.
Uwanja wa ndege wa sasa wa Dubai ambapo uwanja mpya utakuwa mara tano yako