UZUSHI DR Congo: Muasi Sultan Makenga auawa

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kumekuwa na uvumi wa muda mrefu kuwa Bri Gen Sultan Makenga kauawa vitani huko DRC.

Hatimaye Leo zimevujishwa picha za maiti ya Makenga kwenye mitandao ya kijamii.

Itoshe nisema hili ni pigo kubwa sana kwa M23 na kwa Rais Kagame bila kumsahau Lut Gen Kabarebe wa Rwanda.

Brig Gen Sultan Emmanuel Makenga. Ni mtutsi mzaliwa na DRC Jimbo la Kivu ya Kusini. Mji mdogo wa Minembwe.

Makenga ndiye punda wa M23 na CND enzi za Gen Kunda. Punda kwa maana ndiye aliyefanya kazi ngumu zote za uundaji wa CND baadae M23.

Ijapokua ni Mtutsi, Makenga hakupendwa na Kagame. Mtu pekee alikuwa akimpenda Makenga jikoni Rwanda ni Gen James Kabarebe. Na sababu ikiwa Makenga alikuwa msaada mkubwa kwa Kabarebe alipokuwa akiongoza ile Operation Kitona wakati wa vita ya pili Kongo.

Hili ni anguko kubwa sana kwani kwenye makamanda wa M23 ni Makenga ndiye alikuwa na ujuzi mkubwa wa kutumia topography ya Kivu kumanuva vita.

Labda nidokeze 2012 walipokosana Makenga na Bosco Ntaganda ilimchukua siku mbili tu kumuweka kati bw Ntaganda na Ntaganda akakimbilia ubalozi wa US huko Kigali
1657957717778.png
 
Tunachokijua
Mnamo Juni 27, 2022 kulitokea taarifa zikifafanua kuwa Sultan Makenga ameuawa baada ya Helikopta kuwashambulia. Katika Video ya YouTube iliyowekwa Juni 27, 2022 ilieleza:
"Fardc vs M23/ Rwanda: Tetesi za Kifo cha Sultani Makenga Zinaleta Hali ya Taharuki kwa Magaidi wa M23
Kulingana na mwandishi wa habari Christophe Rigaud wa Afrikarabia, kuna tetesi kubwa kuhusu kifo cha Sultani Makenga. Lakini hakuna "uthibitisho wa kuaminika kwa sasa, lakini chanzo cha usalama kimenithibitishia kifo cha Luteni Kanali Youssouf Mboneza na maafisa wengine 3 wa M23 baada ya helikopta ya FARDC kuwashambulia," mwandishi aliandika kwenye Twitter. Vyanzo vingine vimeripoti habari hiyo bila kuthibitisha, na kila wakati wakizungumzia "vyanzo vya usalama." Luteni Kanali Sultani Makenga ni kiongozi wa kijeshi wa Harakati ya Machi 23, kikundi cha waasi kilichoko katika maeneo ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Makenga ni Mutsi kwa asili na alikulia Kusini mwa Kivu. Aliwahi kupigana kwa niaba ya Front Patriotiki ya Rwanda wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda.

Taarifa hiyo licha ya kudokeza fununu zinazoelezea taarifa za kuuawa kwa General Sultan Makenga lakini inakiri kwamba taarifa hiyo haikiwa na uthibitisho wowote.

Upi ukweli kuhusu taarifa hii?
JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali vya habari na kubaini hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichothibitisha kifo cha Sultan Makenga;

Hata hivyo, JamiiForums imebaini kuwa Shirika la Habari la Sauti ya Marekani liliripoti taarfa ya Sultan Makenga kurejea Congo kuendelea mapigani mnamo Julai 5, 2022 ikiwa wiki moja tangu kiongozi huyo kudaiwa kuuawa.

Zaidi ya hayo mnamo Julai 7, 2023 ukurasa wa habari wa The News Times lilitoa taarifa ya Sultan Makenga kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu mgogoro wa Congo.

Hivyo, kutokana na kuwapo kwa uthibitisho wa Sultan Makenga kuendelea na shughuli zake za kijeshi pamoja na kujitokeza kwenye mahojiano, JamiiForums inaona kuwa taarifa zilizomuhusisha kiongozi huyu na kuuawa kwenye shambulizi hazikuwa na ukweli.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom