Bexb
JF-Expert Member
- Oct 24, 2016
- 671
- 1,437
Katika utumishi wa umma haya ni masuala ya kawaida, kama anaona hawezi aende tu DPW aendelee kula shushu mjini hapaimagine unahamishiwa bandari ya bagamoyo ukapambane na majahazi na mangalawa
Katika utumishi wa umma haya ni masuala ya kawaida, kama anaona hawezi aende tu DPW aendelee kula shushu mjini hapaimagine unahamishiwa bandari ya bagamoyo ukapambane na majahazi na mangalawa
Ndomaana wamepewa wachague kati ya TPA /DPW.Si tuliambiwa hawataguswa kabisa?
Hizo zilikuwa danganyà toto tu TPA wanabaki na sehemu ya wavuvi hata ile sehemu ya tics anakuja kupewa Dp na reli ikikamilika bandari za maziwa zinaenda kwa dp salamaleko1. Kama nakumbuka vizuri! Tuliambiwa DP watapewa gati no 7&8 pekee!..sasa mbona hapo wamepewa gati zaidi ya hizo?
2..TPA wamebaki na gati ngapi?.
Competence itawaumbua wengiDP wana world class standard hakuna longo longo kama unajijua wewe unga unga mwana bora bakia TPA....wako very strictly watanzania nawajua wataanza kulalamika soon.....wako atrictly niamini mm
uliambiwa na nani, na lini? ulisoma ule mkataba? "IGA"1. Kama nakumbuka vizuri! Tuliambiwa DP watapewa gati no 7&8 pekee!..sasa mbona hapo wamepewa gati zaidi ya hizo?
2..TPA wamebaki na gati ngapi?.
Na msikiti Utajengwa humo humo ndani, muda utaongea tu hawa Akina Tippp Tipp wamepewa Nchi na Elimu yao tunaenda kuifundisha Shuleni! Mungu atusimamie na hawa Wakoloni waliotugeuza watumwa. DaaaahSifa uwe unaitwa Ally,Hussein, Mohamed,Iddy,Yusufu au abdalah..nyie akina John,Frank,George msijichoshe
Bandari imekuwa kama Simba SC Wana Makolo 🐼Mkuu mbona tangazo lipo wazi au mimi ndio sielewi? Huwezi kuwa mtumishi wa serikali halafu hapo hapo ukawa mtumishi wa DPW. Mumishi anachagua abaki TOA au aende DPW na huo ndio utaratibu na hao watumishi wamepewa elimu na muda wa kuchakata suala hili tangu mapema sana.
Kwa ninachofahu na nilichoelewa ni kuwa Ukiamua kwenda DPW utapewa terminal benefits zote kisha unaajiririwa DPW ambapo huko ni private sector na tunajua huko hakuna mbambamba ni kazi kwa kwenda mbele tofauti na serikalini ambako hata uharibu vipi basi unaangaliwa au watakuhamisha kitengo. Lakini private sector huwa wapo strictly.
Sasa hapo ni uamuzi na uchaguzi wa mwajiriwa mwenyewe abaki au aende lakini hakuna aliyetimuliwa wala kulazimishwa kuchagua atakacho
Wamebaki na ngapi TPA?.Hapana mkuu nadhani umekosea, ni berth 0-7
Kwahyo hakutakuwa na wajiriwa wapya??Mbona siuoni uzi tena?
Wanakuwepo critical areasKwahyo hakutakuwa na wajiriwa wapya??
Sijaona anaeondolewa, au huelewi ulichokibandika?Wale waliokuwa wakitetea kuwa DP World wakija hawatapunguza watu kazi njooni hapa mtueleze. Jamaa ndio wameishauziwa taratibu wanaanza kuondoa watu. Kiko wapi?
---
Tarehe 22 Oktoba, 2023 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliingia Mkataba na Kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai unaohusu uendeshaji wa Gati Na. 0 hadi 3 na Gati Na. 4 hadi 7 za Baridari ya Dar es Salaam kwa kipindi cha miaka thelathini (30). Kutokana na makubaliano hayo yanayohusisha usimamizi na uendeshaji wa maened tajwa, Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam wanapaswa kuchagua kati ya kubaki TPA au kusitisha mkataba wa ajira wa TPA na papo hapo kuajiriwa upya na Kampuni ya DP World.
Menejimenti imekamilisha zoezi la utoaji elimu kwa Watumishi wote wa TPA walio kwenye maeneo husika lililoanza Tarehe 4 hadi 19 Machi, 2024 kwa lengo la kuwapa Watumishi wote uelewa sahihi wa mabadiliko ya uendeshaji yanayoendelea Bandari ya Dar es Salaam. Pamoja na masuala mengine, elimu hii inahusisha mabadiliko ya uendeshaji wa bandari, utaratibu wa makabidhiano, utaratibu wa mtumishi kusitisha mkataba na TРА па раро hapo kuajiriwa upya na Kampuni ya DP World (KWA MTUMISHI ATAKAYEKUWA AMEAMUA KUFANYA HIVYO KWA HIYARI YAKE MWENYEWE BILA KUSHURUTISHWA), pamoja na stahiki ambazo zitatolewa na TPA kwa mtumishi atakayeamua kusitisha mkataba wa ajira wa TPA na kuajiriwa upya na Kampuni ya DP World.
Kwa msingi huo, nawajulisha Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam kuwa, makabidhiano kati ya TPA na Kampuni ya DP World yameanza kutekelezwa. Kwa kuwa zoezi la utoaji elimu kwa Watumishi limekamilika, Watumishi watakaoamua kuajiriwa upya na Kampuni ya DP World wanatakiwa kufika na kuorodhesha taarifa zao Jengo la TPA Makao Makuu, Ukumbi wa Mikutano Ghorofa ya 32 kabla au ifikapo Tarehe 29 MACHI, 2024.