Donald Trump alivyoifadhili harusi ya mtalaka wake kwa mamilioni ya fedha

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,974
6,745
Sijui ni Watanzania wangapi wangeweza kufanya hivyo!

Ivana Trump ndiye aliyekuwa mke wa kwanza wa Donald Trump. Alikuwa wa kwanza kwa Trump, lakini Trump hakuwa mumewe wa wa kwanza wala wa mwisho.

Mume wake wa kwanza alikuwa ni Alfred Winklmayr. Alikubali kuolewa na huyo mwanaume ili aupate Urais wa Austria.

Ndoa yao haikudumu muda mrefu. Ilifungwa mwaka 1971 ikavunjika 1973.

Mwaka 1977, Ivana alifunga ndoa na Donald Trump. Yumkini alitarajia kudumu katika hii ndoa ya pili. Alizaa na Trump watoto 3: Donald Jr (1977), Ivanka (1981), na Eric (1984).

Hata hivyo, hata hii ya pili nayo ilivunjika, mnamo mwaka 1990.

Baada ya kuachana na Trump, Ivana aliolewa na Muitaliano aitwaye Riccardo Mazzuchelli mwaka 1995, na kutalikiana mwaka 1997.

Mwaka huo huo wa 1997, Ivana alianza mahusiano na mwanaume mwingine wa Italia. Hata hivyo, huyo mwanaume aliaga dunia mwaka 2005 kabla hawajafunga ndoa.

Tarehe 12/04/2008, Ivana alifunga ndoa na Muitaliano mwingine aitwaye Rossano Rubicondi. Ivana alimzidi mumewe mpya kwa miaka 23. Alikuwa na miaka 59 na Rubicondi miaka 36.

Miongoni mwa mambo ya kipekee katika hiyo harusi ni pamoja na:

1. Kufadhiliwa na mtalaka wake, Donald Trump. Ilihudhuriwa na watu 400 na kugharimu dola za Kimarekani milioni tatu, sawa shilingi bilioni saba na milioni mia saba na sabini za Kitanzania (exchange rate ya leo).

2. Bintiye, Ivanka alihudhuria kama "her maid of honor".

3. Ilifungishwa na wifiye wa zamani (dadaye Donald Trump), Jaji Maryanne Trump Barry.

4. Bibi harusi alikuwa mkubwa kwa bwana harusi kwa miaka 23

5. Ilifanyikia kwenye ukumbi /jengo linalomilikiwa na mumewe wa zamani, Donald Trump.

Pamoja na "upekee" wake, ilidumu kwa muda mfupi sana. Ilivunjika mwaka 2009.

Rubicondi aliaga dunia 29/10/2021, akiwa na miaka 49, na Ivana alifariki 14/07/2022, akiwa na miaka 73. Alizaliwa 20/02/1949.

Kwa nini Trump aliamua kufadhili harusi ya mtalaka wake?

1. Upendo?

2. Ukarimu?

3. Kujiongezea umaarufu?

4. Alitaka kuwaridhisha watoto wake, hasa binti yake, Ivanka?

5. Kejeli kwa Ivana na mumewe mpya?
 
Wenzetu wanaoana na kuachana vizuri, then wanapata wengine huku wakiendelea kutokuwa na chuki na ma X wao

Njoo sasa huku kwetu wa kwa mtogole.

X atatukanwa matusi yote mabaya na mazuri
 
Back
Top Bottom