Dodoma: Mbunge apendekeza wanaobaka wapewe Pombe za kupunguza nguvu za kiume

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,512
220,207
Mwantumu Dau Haji ambaye ametajwa kama Mbunge wa Viti Maalum , amependekeza bungeni kwamba , wale wote wanaobakwa wakishakamatwa wapewe pombe ya kupunguza nguvu za kiume ili wasibake tena .

Toa maoni yako .

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app

===========

Mbunge wa viti maalum (CCM), Mwantumu Dau Haji ametaka wanaume wanaobainika kufanya ukatili wanawake na watoto wamepewe pombe zinazopunguza nguvu za kiume ili wasiweze kufanya vitendo vya ulawiti na ubakaji.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Mei 18, 2023 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Watoto na Makundi Maalum kwa mwaka 2023/2024.
Amesema wanaokamatwa kwa kufanya vitendo hivyo bado wanapewa dhamana na kuhoji kama kwa kufanya hivyo tatizo litatatulika.

“Sijui kwamba aende akabake tena, sijui aende kujitetea kivipi…Na anapochukuliwa dhamana anakwenda zake nje anakwenda kufanya vitendo vingine bado hili suala halijafikia malengo,”amesema.

Amenukuu Mbunge wa Momba (CCM) Condester Sichalwe akisema kuna pombe ambazo wanaume wakinywa zinakwenda kupunguza nguvu za kiume.

“Kwanini hawapewi, ili wakitoka hizi nguvu za kiume ili tukaondokana na hili suala tuliokuwepo nalo hapa nchini? Wapewe wanywe maana kuhasiwa hawataki kuhasiwa. Wapewe hizi pombe wakatike nguvu za kiume maana tunaweza kupata suluhisho,”amesema.

MWANANCHI
 
Ukishamuasi anakuwaje sasa?
Unataka kuongeza wanachama wa chama kileee wewe
Waache watu waishi kaka
 
Hivi hizi pumba huwa wanaongea wakichangia kitu gani?? Ni kitu gani kinawasukuma wabunge kusimama na kutoa uharo wa aina hii?

Anyway, hawa ndio wawakilishi wa wananchi, kwa sababu hata wananchi wenyewe wengi wao ni mbumbumbu.

No wonder serikali inalitumia bunge kama 'rubber stamp' tu, welevu wachache wajinga wengi. Na hata welevu inabidi wajifanye wajinga ili ku survive. Mambo ya kipumbavu kabisa.
 
Back
Top Bottom