Digital channel moja picha mbili tofuati ( Easytv vs Startimes)

Tumsifu Samwel

JF-Expert Member
Jul 30, 2007
1,407
159
Habari wakuu? mimi ni mtumiaji wa king'amuzi cha Eastv na jirani yangu anatumia cha Startimes, jana nilitaka kutizama UEFA Champions League na kwa tz channel inayorusha matangazo ya mchezo huu ni DTV pekee kama sijakosea, na ilipofika Saa 9:30PM niliweka DTV ili nitazeme mpira nikakuta kuna mwachambuzi wa mpira wa siku nyingi DK licky akiwa na mtangazaji wa DTV wakiuzungumzia huo mchazo wa jana kati ya Man United na Galatasaray

Baada ya mda mchache walisema mpira unaanza na wapate matangazo kadhaa kabla ya mpira kuanza, baada ya matangazo kwisha nilishangaa wanaleta miziki badala ya kutuonyesha mpira, kwa jirani yangu nikasikia anatizama mpira ikabidi ni niende kutizama kwake, kilicho nishangaza ni kwamba alikuwa anatizama huo mpira kupitia DTV (yeye anatumia Startimes na mimi ni Easytv) ambayo kwangu ilikuwa inapiga mziki badala ya kuonyesha mpira. Na baada ya half time wachambuzi walirudi tena hewani na, nikarudi kwangu na kukuta pia wachambuzi wako hewani ila kipindi cha pili kilipo anza mimi niliwekewa nyimbo wakati jirani yangu aliunganishwa na mpira huo.

Kiukweli nilichindwa kuelewa ina kuwaje tutizame channel moja wote na wingine aone kitu tofauti na ninacho kiona mimi ebu wakuu nielewesheni hapa


 
Back
Top Bottom