Diamond kaangushwa na mameneja wake sio Wanaharakati

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,289
22,822
Nawasalimu katika jina la Chama Cha Mapinduzi chama kiendelee. Kabla baadhi yenu hamjaanza kunisumbua kutaka nitoe maoni yangu kuhusu kushindwa kwa komredi Simba kwenye tuzo za BET, nimeona niyatoe mapema. Kama kawaida maoni yangu ndo yatakuwa msimamo wa JF. Soma kwa makini.

Kwanini kashinda Burna Boy na sio kada wa CCM Komredi Diamond Platinumz? Ieleweke Meneja wa Burna Boy ni mama yake mzazi. Unaweza ukakurupuka na kudhani labda Mama Dangote naye awe meneja wa mtoto wake ili kurahisisha kazi. Tuzingatie kuwa Mama Burna sio mgeni kwenye kazi yake ya umeneja. Huyu mama ni binti wa Benson Idonije ambaye alikuwa meneja wa mwanamuziki mkubwa kuwahi kutokea Afrika, komredi Fela Kuti. Mama Burna ana Masters degree toka Chuo Kikuu cha Port Harcourt. Huyu mama huzungumza kwa ufasaha lugha ya kiingereza, kifaransa, kijerumani, kiitaliano na kiyoruba. Amefundisha kifaransa kwa miaka 10 kwenye Chuo Kikuu cha Port Harcourt na kustaafu 2018. Kimsingi Mama Burna ana CV ya kutisha pia kakulia kwenye familia ya meneja. Hiyo kazi ipo damuni.

Pamoja na Burna Boy kupata Meneja mwenye viwango vya kimataifa bado tunaambiwa nguli P Didy (Sean Puffy Combs) ni meneja wake kwa upande wa Amerika. CV ya Diddy kwenye muziki ndani ya USA inaeleweka yaani hakuna haja ya maelezo. Tukiachilia mbali mameneja wa Burna, tukumbuke hata Burna ni msomi wa Chuo Kikuu.

Komredi Simba huenda ana kipaji kikubwa kuliko washindani wake lakini tunaona menejimenti yake ni dhaifu kuweza sawa na ushindani wa mameneja wengine. Mimi naona inabidi tukubaliane kwamba kijana aajiri meneja atakayeweza kwenda sawa kimataifa. Mameneja waliopo ndo uwezo wao ulipofikia hatuna cha kuwalaumu zaidi ya kuwapongeza. Ila nao waukubali huu ukweli mchungu. Meneja mwenye elimu ya darasa la saba ni ngumu sana kumvusha msanii wetu. Meneja anatakiwa awe mbali kimaono kuliko msanii. Lakini WCB inaonekana msanii ana akili kuliko mameneja.

Nimalizie kwa kusema kwamba hawa wa Twitter na wanaharakati uchwara kama Maria Sarungi & company hawakuwa na uwezo wowote wa kuzuia Simba kupata tuzo. BET haipo kisiasa. Na kama kungekuwa na jambo baya kwa vyovyote wangeuliza ubalozi wa USA nchini. BET haina kipengele cha siasa kwenye shuguli zake.
 
Diamond na wasanii wengine kina Harmonize & Kiba kwasasa hawawezi kumshinda Burna Boy hata wakiwa na mameneja malaika, bado wanatakiwa kukuza sana sanaa zao ziwe za kimataifa zaidi, hawa wasanii wetu mwisho wao kwasasa ni East Afrika tu japo wana makeke kibao lakini ukweli ndio huo.
 
Siku zote ni ngumu sana msanii anayeimba nyimbo zake kwa kiswahili kumshinda msanii anayeimba nyimbo kwa lugha ya Malkia Elizabeth wa Buckingham palace. Mshawishini Mond awe anatunga na kuimba nyimbo zake kwa lugha ya malkia ndiyo ataweza shinda tuzo za maana,vinginevyo mtasubiri sana.
 
Mtaiongea mengi sana mwaka huu lakini huo ni wivu wa maendeleo aliyonayo diamond hamuwezi kumfikia hata siku moja kwa chuki hizo badirikeni
 
Unajua asili ya BET awards?ni mambo ya siasa baada ya kuona wazungu wanawabagua blacks katika mambo ya sanaa kama kutopiga nyimbo za blacks kwenye Tv na radio,so BET wanapinga udhalimu,daimond yupo upande wa wadhalimu ndio maana kaangukia pua na manguo yake kama gods must be crazy
 
100% well said.

Meneja ni mbunge?

WCB iende mbali kuajiri management yenye weledi na iachane na management yenye vinasaba vya siasa.

WCB waache kuchanganya siasa na muziki wao, wajifunze wenzao walivyofanikiwa kimataifa.
 
Back
Top Bottom