Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,120
Na inaonekana ana jicho limeiva kama nyanya si ajabu kavuta misokoto kadhaa
JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani limeshikilia dreva wa kampuni ya Ahmed Trans lenye namba za Usajili T586 AJH linalofanya safari ya kusafirisha abiria kati ya Mbeya na Tanga Rajab Omari baada ya kumkuta amelewa chakali huku akiwa amebeba abiria tayari ya kwa safari ya kutoka Mbeya kwenda Tanga.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya Mkuu wa Oparesheni ya Trafic kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ACP Nassor Sisiwah amesema wakiwa katika zoezi la ukaguzi wamemkamata Dereva huyo na baada ya kumpima wamemkuta na kileva 450 .3 ml/gm kinyume cha sheria.