SoC03 Demokrasia ya kweli

Stories of Change - 2023 Competition
Jun 8, 2023
4
1
Tanzania ni moja ya nchi duniani inayotumia mfumo wa uongozi wa demokrasia. Na mfumo huu ulianza haswa kuvuma miaka ya 1990 baada ya kurudishwa mfumo wa vyama baada ya miaka thelathini katika kipindi cha ukoloni lakini licha ya hivyo kwa sasa kumekuwa na malalamiko au tuhuma mbali mbali kutoka kwa wananchi kuwa Tanzania haifwati sifa za na sheria za demokrasia ya kweli nazo ni kama ifuatavyo;

1. KATIBA
katiba ya ni moja ya muhimbili mkubwa na unaotegemewa katika suala la uongozi serikalini, lakini katiba ya Tanzania imekuwa ikishangaza sana wanademokrasia duniani kwa sababu ni katiba ambayo iliweza kuandikwa katika kipindi cha mfumo wa chama kimoja miak ya 1970 lakini ndiyo hiyo hiyo inayotumika mpaka hivi leo.

2. UHURU WA KUJIELEZA
Tangu demokrasia ianzishwe mpaka hasa kwa miaka ya hivi karibuni wananchi na viongozi mbali mbali wamekuwa wakipata vitisho na adhabu mbali mbali pale ambapo wanaikosoa serikali iliyopo madarakani,pia kumekuwa na vitisho mbali mbali kutoka serikalini pale ambapo vyama pinzani katika nchi ya Tanzania kukataliwa kufanya mikutano ya adhara,pia kumekuwa na figisu mbalimbali za viongozi wa upinzani kutolewa relini pale ambapo wanakuwa mmstari wa mbele katika kuikosoa serikali na mengine mengi yanayo fanana na haya.

3. UCHAGUZI
Pia katika suala la uchaguzi mpaka hivi sasa umekuwa sio wa kweli na wa haki kutokana na sababu mbali mbali zinazojitokeza katika kipindi cha uchaguzi kama vile msi u ulio pita wa uchaguzi wa serikali za mtaa vyama pinzani kama vile CHADEMA viligoma kushiriki katika uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali na kufanya asilimia zaidi ya tisini ya viongozi wa mitaa kushikiriwa na chama tawaka ambao wamepita bila kuchaguliwa, pia kutokana na changamoto zilizotokea katika suala la uchaguzi wa wabunge mwaka 2020 asilimia zaidi ya 99 ni wa chama tawala na wale ambao wanasemekana ni wa vyama pinzani ni wabunge ambao wapo bungeni na serikali inawatambua kabisa na wanafanya shughuri zote za kibunge lakin wabunge hao hawatambuliwi na vyama vyao kuwa ni wabunge, Je kwa namna hii Tanzania ni nchi anayofwata misingi ya kidemokrasia ya kweli?

Kwangu mimi nitaweza kusema hapana, na vitu vyote hivi vinavyotekea vimeweza kusababishwa na sisi wenyewe wananchi kwasababu nchi zote ambazo zinaendeshwa kwa mfumo wa kidemokrasia na kuendelea mpaka hivi sasa ni nchi ambazo wananchi wake ndio waliweza kupambania na kuweza kufanya mabadiriko katika suala la uongozi na kuanzisha mfumo wa demokrasia, mfano mzuri ni kwa nchi kama vile nchi ya uingereza ni nchi ambayo demokrasia ilianza kuvuma miaka ya 1600 pale ambapo familia ya kifalme ya Stuart ilipo anza kuzidisha mabavu katika kuliongoza taifa ndipo wananchi walipo anza kupinga mfumo wa kifalme katika suala lauongozi kwa kufanya mapinduzi na mapinduzi hayo asilimia kubwa yalifanywa na wananchi hasa wale wa hari ya chini pia tukienda kwa nchi Kama Marekani ambayo watu wengi wanapenda kuiita mama wa demokrasia ni nchi ambayo ilitawaliwa kama sisi tu lakini tofauti yetu na wao ni kuwa wenyewe baadhi ya viongozi wa uingereza waliokuwa nchini humo walipo choka kutawalia na serikali ya manyanyaso na unyonyaji ya uingereza wakaamua nao wajitafutie uhuru.

Kutokana na hivyo basi ili tuweze kupata viongozi walio bora na wawajibikaji hasa katika nchi ya Tanzania ni pale ambapo sisi kwananchi tutaamua kuongozwa katika misingi ya demokrasia ya kweli, mfano viongozi wa serikalini ili wawajibike ni lazima waweze kukosolea pale wananchi wanapoona kuna mapungufu, pia sisi Kama wa Tanzania inabidi tukubaliane sisi kama sisi kuwa tunauelewa mzuri kuhusu demokrasia kwa sababu demokrasia invyooanzishwa Tanzania hasa katika nguzo ya mfumo wa vyama vingi mfumo huu haukuanzishwa kwa sababu ya mapendekezo ya wananchi bali ulianzishwa kutokana na kufwata sheria za mashirika ya fedha duniani ili tuweze kupata mikopo itakayo tuwezesha kujikwamua katika anguko la kiuchumi, na ndio maana baba wa taifa alivyomtuma nyalali kwa wanachi ili apate maoni kama watanzania walikuwa tayari kwa mfumo wa vyama vingi asilimia zaidi ya 99 ya watanzania walisema hawapo tayari na wabaki katika mfumo wa chama kimoja, kutokana na hivyo basi kwa maana hiyo mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania haukuanzishwa kwa sababu ya wananchi na viongozi wake Bali ulianzishwa kutokana na sheria zilizoweza na mashirika ya fedha ili tuweze kupata misaada. Vitu vyote hivi na ndio maana vimesababisha mpaka hivi sasa tuweze kuwa na katiba ya chama kimoja.

Rai yangu ni kwamba ili tuweze kupata maendeleo katika nchi ya Tanzania inabidi tuweze kupata viongozi walio bora na wawajibikaji na viongozi hao wataweza kupatikana pale ambapo tutakuwa na mfumo bora wa uongozi na kwa sasa mfumo bora wa uongozi kwa sasa unaofaa ni demokrasia na sio demokrasia tu bali ni demokrasia ya kweli, na maana halisi ya demokrasia ya kweli itaweza kuonyeshwa na sisi wenyewe wananchi wa Tanzania na haitoweza kuonyeshwa na sisi watanzania kwa kupiga kura tu Bali kupiga kura kwa kumchagua kiongozi aliye bora kwa kuto jali kuwa amerokea katika chama chako ,cha baba yako au unachokipenda,Bali utamchagua kiongozi kwa sababu umemuona kuwa ndiye kiongozi atakayeleta maendeleo katika nchi.Piah sisi Kam wenye nchi ambao mtu yoyote yule ambaye ni mtanzania anaweza kushika nafasi yoyote katika ngazi ya serikali tuweze kuwa na misimo ambayo viongozi waliokuwa madarakani wanaweza kuhamasika katika uwajibikaji na kuiongoza nchi vizuri.

Kwa kumalizia ni ivi ushawahi fikiria kuwa baad ya miaka elfu moja je,vizazi katika nchi ya Tanzania na Afrika kwa ujumla tutakuwa viongozi wa dunia au bado tutakuwa tunaongozwa kwa kutegemea kila kitu kutoka kwao Kama haupo tayari kwa kiizazi chako cha baadae kuwa Kama hivy ulivyo basi anza kuchukua hatua sasa bila kujali kesho yako itakuwaje ,Asante na sote tushirikiane katika kijenga Tanzania inayofuata misingi ya demokrasia ya kweli ili tuweze kupata viongozi walio bora katika uwajibikaji wa kulitumikia taifa katik ukweli na haki ili tusibaki hivi tulivyokuwa na hatta milele.
 
Back
Top Bottom