ISRAEL JR
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 1,487
- 687
Katika Ukurasa wake wa tweeter Mhe David Kafulila ameandika haya:-
************************************
"Kwasasa Umuhimu wa kutumia nishati mbadala hauna mbadala,
Tanzania sasa ni miongoni mwa nchi 5 duniani kwa kasi ya ukataji miti.
Nchi zingine ni pamoja na Brazil, DRC, Indonesia na Angola.
Tunapoteza miti eneo la hekta 496,000 sawa na kilomita za mraba 4960.
Hii ni sawa na kupoteza eneo kubwa zaidi ya mara tatu ya Jiji la Dar es Salaam kila mwaka!"
**********************************
Kama kweli Tanzania kila mwaka inapoteza eneo la miti lenye Ukubwa mara tatu zaidi ya Dar es salaam kwa kukata miti hii ni ripoti ya kutisha sana,
Hili si jambo la CCM, ACT,CUF ,TLP Wala CHADEMA Kila mmoja lazima asimame kuzuia ukataji wa miti kiholela na ahamasishe utumiaji wa Nishati Mbadala na tupande miti ya kutosha sehemu tunazoishi na kufanya kazi.