HPAUL
JF-Expert Member
- Jan 18, 2011
- 410
- 567
Leo upande wa mashtaka umefunga ghafla kesi ya ugaidi inayowahusu washtakiwa wanne akiwemo Freeman Mbowe.
Katika hali ya kushangaza shahidi muhimu ambaye akitajwa karibu kila siku na mashahidi wa upande wa serikali DCI Boaz hajaitwa mahakamani kutoa ushahidi.
Ikumbukwe huyu ndiye aliyepokea taarifa kutoka kwa Luteni Urio, juu ya kuwepo mipango ya ugaidi, na yeye aliye andaa mpango kazi wa awali wa kesi hii. Boaz alitakiwa kuja kuieleza mahakama ni kwa jinsi gani aliiona hii kesi ni ya ugaidi, alitakiwa kuunga mkono ushahidi wa Urio na kuthibitisha kwamba kweli Urio alifika ofisini kwake, maana hapo Kuna utata mkubwa, alitakiwa kuieleza mahakama ni kwa Nini alikubali mpango wa kuharibia maisha makomandoo watatu ambao walikuwa na kazi zao, warubuniwe na Urio kwamba Kuna kazi ya ulinzi VIP kumbe wanatumbukizwa shimoni na kubambikiwa ugaidi, kifupi bila Boaz kutoa ushahidi muunganiko wa kesi nzima unakosekana.
Hii haijatokea kwa bahati mbaya, pengine hii kesi ni mchongo hivyo kumleta DCI mahakamani na kudhalilishwa siku 3 mfululizo ni Kibatala itakuwa ni aibu kwa taifa, lakini majibu mazuri zaidi wanayo upande wa mashtaka.