David Silinde hakuwa mroho, anastahili sifa

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,842
20,561
Mwaka 2010 kijana David Silinde aliibuka mshindi wa kiti cha ubunge katika jimbo la Mbozi Magharibi kupitia CHADEMA. Hakuna shaka yoyote kwamba wabunge wakiwa ndani ya majimbo yao huwa wana sehemu ambazo ndio 'roho' zao, yaani ngome wanazozitegemea. Kwa upande wa jimbo la Mbozi Magharibi, ngome kuu ya Silinde na CHADEMA ilikuwa ni mji mdogo wa Tunduma na advantage yake ni mkusanyiko wa wafanyabiashara wengi.

Mwaka huu 2015, jimbo la Mbozi Magharibi liligawanywa kuwa majimbo mawili, yaani Tunduma na Momba. Pamoja na kuwa Silinde alifanya mambo makubwa pale Tunduma na kuifanya CHADEMA kujiongezea umaarufu, Silinde aliwaomba wana Tunduma wampe ruhusa akagombee jimbo lililogawanyika la Momba, tena ambako hakukuwa na ngome ya CHADEMA na wala haikuwa rahisi kwa wapinzani kushinda kutokana na CCM kumuweka mgombea maarufu aliyewahi kushika wadhifa wa uwaziri, Dr Lucas Siame.

Kwa nini Silinde alichagua Momba na sio kwenye 'mteremko' Tunduma? Ni uzalendo wake kwa chama chake kwani alijua walau yeye anaweza kupimana ubavu na CCM kuliko kumuachia yosso mwingine. Alijua Tunduma itaenda CHADEMA tu, ila alitaka na Momba iende CHADEMA pia kwa mapenzi yake ya kuongeza viti vya ubunge kwa CHADEMA.

Si rahisi mbunge aliyeonja posho akakubali kuacha kwenda kugombea sehemu yenye mteremko kwake akachagua kwenda kupambana kwingine kwa maslahi ya chama chake. Silinde amepambana na ameweza kumuangusha Siame, na majimbo yote mawili yaliyogawanywa yaani Tunduma na Momba yameenda CHADEMA. Kama vile haitoshi, ushawishi wake umesababisha hata jimbo lingine la jirani la Mbozi lililokuwa chini ya Godfrey Zambi wa CCM kuangukia mikononi mwa CHADEMA pia.

David Silinde is my hero!
 
Hongera zake na tunahitaji vijana kama hawa sababu alijitoa ili kujenga chama sehemu za ndani zaid na lengo limefanikiwa kitu ambacho vijana wengi hawapo tayari kwenye hilo.
 
Mungu amsaidie, kisha ampe afya, ampe familia nzuri ili awatumikie vizuri watanzania.
 
Ubungo - Kibamba,
Tunduma na Momba.

Wapi kwingine MCC walifanya uchakachuzi wakafanikiwa au kuangukia pua?
 
Wanao sema Tz ni nchi maskini haiwezi toa elimu bure waseme ndiyo Ndiyoooooooooooooooooooooooooo waliosema ndiyo wameshindaaa Haya tuendelee KATIBU
 
Punguzeni chuki zenu kwa Zitto.

Zitto pekee ake ni sawa na wabunge wote wa ukawa.

Mimi nakubali Zitto anawazidi wabunge wengi wa ccm kasoro Serukamba. Kwa kweli ccm nzima wabunge wake awe wa jimbo hata viti maalum hayupo wa kutia mapua kwa Serukamba kwa sifa yoyote ile. Mwingine wa aina ya Serukamba angekuwa Deo Filikunjombe kama mungu angemwacha hai. Ukawa hayupo m-bunge wa kumlinganisha na Zitto wanamzidi kwa mbali.
 
Mimi nakubali Zitto anawazidi wabunge wengi wa ccm kasoro Serukamba. Kwa kweli ccm nzima wabunge wake awe wa jimbo hata viti maalum hayupo wa kutia mapua kwa Serukamba kwa sifa yoyote ile. Mwingine wa aina ya Serukamba angekuwa Deo Filikunjombe kama mungu angemwacha hai. Ukawa hayupo m-bunge wa kumlinganisha na Zitto wanamzidi kwa mbali.

uko sahihi kabisa mkuu ndy maana wanazidi kuongezeka bungeni kila tukifanya uchaguzi sababu ya kazi ya njema
 
Back
Top Bottom