Chimbuko la usomaji huu wa saa ni nini?

kwa nn saba isomwe 1???
Tofautisheni AM(ante meridian) na PM (post meridian).Huu ni mstari wa Greenwich meridian.Huu mstari umepita wingereza mji wa Greenwich ukakatiza Ghana.Longtude yake ni degree 0
7.00am maana yake masaa saba yamepita baada siku kuanza hiyo ni asubuhi.Ikifika mchana saa saba inakuwa 1.00pm yaani lisaa limoja limepita baada ya PM.Usiku saa moja inaandikwa 7.00pm yaani masaa saba yamepita baada ya PM
Kumbuka AM inaanzia saa sita usiku hadi saa sita mchana.
Infact wazungu wako more scientific wakizingatia mzunguko wa dunia.
 
Tunamshukuru mwanao ameelimisha wengi.Ningemjua ningempa soda
Nina uhakika kuna maproffessor hawakujua hili
Habar wanajamvi
Leo nmekutana na changamoto baada ya mwanang kuniuliza swali ambalo sikuwa na majib ya kuridhisha. Swali lenyew n huu utaratibu wa kusoma saa, yaan kwa mfano kwa kama n saa saba mchana, huandikwa 1 badala ya 7.
Huu utamadun ulianzia wap na kwa nn??
Ahsanten na karibun san Wajuv mnijuze
 
Siku nyingine mbeleni dogo atauliza 15:30 au 2100hrs ni saa ngapi na Mbona kwenye saa Sioni?
 
kwa nn saba isomwe 1???
Hiyo ni saa 1, na wazungu wanasoma hivyo hivyo 1, wewe ndo wakosea kusoma saa Saba. Labda nikuulize, kama usiku ni saa sita, kwa nini basi iwe siku inabadilika hiyo saa sita inapofika wakati sita iko katikati??

Jibu ni kua pale siku inapobadilika ni saa 12 au 24 ndo saa zimefikia mwisho. So atakaeita pale saa 12 au 24 yuko sahihi zaidi kuliko wewe utakaeita saa sita.
 
Habar wanajamvi
Leo nmekutana na changamoto baada ya mwanang kuniuliza swali ambalo sikuwa na majib ya kuridhisha. Swali lenyew n huu utaratibu wa kusoma saa, yaan kwa mfano kwa kama n saa saba mchana, huandikwa 1 badala ya 7.
Huu utamadun ulianzia wap na kwa nn??
Ahsanten na karibun san Wajuv mnijuze
Huo ni mpango wa Devils worshiper . Ndio maana kwa kila saa wameongea Masaa 6. Mfano saa 6 mchana inaandikwa 12. 12-6=6. Mfano saa 1 asbuhi inaandikwa 7. 7-1=6. Huu ni matumizi ya Namna 666 au namba ya Anti christ. Kwann wasingeongeza saa 8. . ?
 
Kiswahili ndo kimeleta huu ufala, 07:00am ni seven a.m, yaani masaa 7 toka siku ianze. sasa mswahili akasema saa moja kamili asubuhi. Inshorti siku ya kiswahili inaanza asubuhi siyo saa sita usiku
Wewe ndiyo fala aisee.
 
waswahili, wahabeshi huhesabu siku kuanzia saa moja asubuhi, pale jua linapochomoza hapo wao ndio husema saaa moja na siku imeanza, wazungu siku inaanza usiku, saaa tumia akili siku inaanza jua likichomoza ama usiku wa giza tii usio na alama yeyote
siku si ina masaa 24 siku inaisha alfajiri, na nyingine inaanza kukipambazuka kipi kigumu kuelewa
Now look how we contradict ourselves!

Tunahesabu siku kuanzia saa 1; JUA LINPOCHOMOZA! Hapo hapo kuna majira mengine ya mwaka, jua huchomoza kabla ya "saa 1 ya Kiswahili" lakini bado hatuwezi kuita saa moja!! Na nyakati zingine jua huchomoza baada ya saa moja, na bado hapo linapochomoza hatutaita saa moja!!

Sasa ukisikia kukosa uniformity, ndo huko!!

Again, Waswahili na sisi huwa tunasherehekea Mwaka Mpya!! Wakati siku za kawaida tunaanza siku saa 1, siku ya mwaka mpya tunaanza siku at 00:00 (yaani saa 6 usiku) sawa na kwingineko duniani ambako hatutumii timing yao! Sasa kama tunaamini siku inaanza saa 1, kwanini na mwaka mpya tusiukaribishe saa 1?!
 
sasa kwanini tuhesabu siku kwa mtindo wenye manufaa kwa wasweden wakati sie siku zetu zimekaa kwa kueleweka kuwa saa moja jua litachoza saa kumi na mbili tutazama
ni kwa sababu mswahili hajawahi kuwa na kitu chake, vyoote ameiga isipokuwa umbea, uchawi na ushirikina.
 
ni kwa sababu mswahili hajawahi kuwa na kitu chake, vyoote ameiga isipokuwa umbea, uchawi na ushirikina.
wewe ndio hujui waswahili, mnaona walokosa elimu kwnye miji yetu ya siku hizi kuwa ndio waswahli ilhali waswahiki wenyewe walikuwapo mamia ya miaka kabla ya leo
 
Now look how we contradict ourselves!

Tunahesabu siku kuanzia saa 1; JUA LINPOCHOMOZA! Hapo hapo kuna majira mengine ya mwaka, jua huchomoza kabla ya "saa 1 ya Kiswahili" lakini bado hatuwezi kuita saa moja!! Na nyakati zingine jua huchomoza baada ya saa moja, na bado hapo linapochomoza hatutaita saa moja!!

Sasa ukisikia kukosa uniformity, ndo huko!!

Again, Waswahili na sisi huwa tunasherehekea Mwaka Mpya!! Wakati siku za kawaida tunaanza siku saa 1, siku ya mwaka mpya tunaanza siku at 00:00 (yaani saa 6 usiku) sawa na kwingineko duniani ambako hatutumii timing yao! Sasa kama tunaamini siku inaanza saa 1, kwanini na mwaka mpya tusiukaribishe saa 1?!
mwaka mpya tunao sherehekea sio mwaka mpya wa waswahili huo ni mwaka mpya wa wazungu. nenda zenji kuna sikukuu inaitwa mwaka kogwa huo ndio mwaka mpya wa mswahili
 
Mi saa yangu siku zote saa 8 mchana inasomeka 8 vile vile sitaki kupelekeshwa kipumbavu mimi.Eti huwa wananishangaa yaa 1:isomeke 7 kwani mi profesa Kabudi
 
mwaka mpya tunao sherehekea sio mwaka mpya wa waswahili huo ni mwaka mpya wa wazungu. nenda zenji kuna sikukuu inaitwa mwaka kogwa huo ndio mwaka mpya wa mswahili
Na hii kalenda ambayo kwa mbwembwe zote huwa tunaandika, mathalani kama leo ni 14/06/2019 na ndio pia inayoleta huo mwaka mpya! Je, hiyo kalenda ni ya Waswahili? And assume umeandika ripoti kwa ajili ya Waswahili na umeqandika saa 7 zilizopita ( saa 11 alfajiri ya Kiswahili), na pamoja na mambo mengine, kwenye ripoti husika unatakiwa kuandika tarehe na siku. Je, siku husika ungeandika ni Ijumaa au Alhamisi?
 
kwa ziada, waarabu waajemi na wayahudi wanaanza kuhesabu siku saa moja usiku.
ndio maana pale mwezi unapoandama huwa jioni na watu hupiga azana kumaanisha siku ya idi imefika, yani ile jioni ya saa kumi na mbili na saa moja wao ndio tarehe mpya huanza

pia, waswahili siku ya kwanza ya wiki ni jumamosi, wakati waarabu na wayahudi siku ya kwanza ni jumapili, wakati huohuo wazungu siku ya kwanza ya wiki ni jumatatu

Babeli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom