CHADEMA ni msumari wenye kutu, haumezeki

Kyenyabasa

JF-Expert Member
Mar 8, 2023
248
712
Mimi si mwanasiasa ila ni Mtanzania ninayenufaika na siasa. Kwa umri wangu mdogo, nimeona vyama vingi vikifa ikiwemo CUF, chama ambacho nilikipenda sana, ila baadaye nikaanza kuvutiwa na smartness ya Chadema, ingawa si mwanachama.

Kwa mtazamo wangu, Chadema imejengwa kwenye msingi imara sana, hivyo si rahisi kuiangusha. Kuhusu maridhiano, naunga mkono kwa sababu harakati bila mazungumzo zinaweza zisikupatia kile unachostahili, hasa kama yule unayepambana naye ana nguvu nyingi pia.

Kwa hali ilivyo, maridhiano yakizaa katiba mpya, basi Mbowe, anayebezwa, atakumbukwa miaka mingi mbele, na hiki ndicho wahafidhina wengi ndani ya CCM na Chadema hawataki kitokee, kwa sababu kitainyanyua sana jina la Mbowe. Mengine yote yasemwe, ila maridhiano ni kete muhimu sana.

Chadema ni watundu mnooo huwezi kuwameza kirahisi, ndio maana nimewafananisha na msumari wenye kutu. Hawa watu ni wahuni, huwezi kuwaua kirahisi. Maslahi ya Chadema na CCM yabaki kwanza chini, ila ya Tanzania yetu yawekwe mbele.

Hongera Samia na Mbowe.
 
Kwa Nguvu aliyotumia Yule dhalimu akiongozwa na Chuki aliyokuwa nayo kutaka kuifuta Chadema na akaiacha ikiwa bado imara bado, hakuna tena wa Kuiua.

Maana jamaa alianza na wanachama,akawavuna walionunulika kwa maneno na ulaghai,akaja wabunge,akahakikisha anahonga vyeo na akanasa waliotanguliza matumbo yao,waliokataa walipigwa risasi na misumari,wengine wakavuliwa ubunge kwa lazima,wengine wakakimbilia kuponya majeraha nje ya nchi,akaja kwa viongozi wa kati ,hapo zikapigwa mbinu na mikwara,kesi na ahadi za vyeo,akanasa wachache,akaja uongozi wa Juu kabisa,hapo akaongeza nguvu,vyombo vyake vyenye nguvu na anavyoviamini mno vikabuni kesi ngumu na tata huku walengwa wakitakiwa kuungana nae au wakumbane wa kesi ngumu za ugaidi na uhujumu uchumi akakwama,akaona haitoshi,akafunga akaunti zao binafsi.

Akaja kuilenga taasisi nzima na na mfumo wake,akatafuta kosa la kuifuta akashindwa,akapiga marufuku mikutano ya hadhara,ilimradi wasisike kabisa,akafanikiwa ila Chadema wakaja na "Chadema ni msingi' kuimarisha chama huko ndani ndani,yeye hakujua.

Akaona bado wapo active mitandaoni,akafunga baadhi ya mitandao,mingine akashindwaiwemo JF ila wamiliki chamoto walikiona.

Akasubiri mbinu kuu,tukaingia uchaguzi mkuu chama kikiwa na Majeraha kibao,akahakikisha anawaengua wagombea wote wa ubunge,akafanikiwa,akajaribu kumuengua mgombea wa Uraisi akakwama,alipoona moto wake mkali,akaamrisha kura zote zitakazopigwa kwa Chadema zihamishiwe kwake wabakiziwe chache za ushahidi,akafanikiwa kwa hilo,ndio ule ulioitwa "UCHAFUZI".

Hapo akahakikisha Chama hakina ruzuku ili life kifo cha taratibu,Chadema wakaibukia mitaani na 'join the chain'

Alipoishiwa mbinu alikufa yeye akaicha Chadema ikichanua kama tumaini jipya la Tanzania.
 
Mimi si mwanasiasa ila ni Mtanzania ninayenufaika na siasa. Kwa umri wangu mdogo, nimeona vyama vingi vikifa ikiwemo CUF, chama ambacho nilikipenda sana, ila baadaye nikaanza kuvutiwa na smartness ya Chadema, ingawa si mwanachama.

Kwa mtazamo wangu, Chadema imejengwa kwenye msingi imara sana, hivyo si rahisi kuiangusha. Kuhusu maridhiano, naunga mkono kwa sababu harakati bila mazungumzo zinaweza zisikupatia kile unachostahili, hasa kama yule unayepambana naye ana nguvu nyingi pia.

Kwa hali ilivyo, maridhiano yakizaa katiba mpya, basi Mbowe, anayebezwa, atakumbukwa miaka mingi mbele, na hiki ndicho wahafidhina wengi ndani ya CCM na Chadema hawataki kitokee, kwa sababu kitainyanyua sana jina la Mbowe. Mengine yote yasemwe, ila maridhiano ni kete muhimu sana.

Chadema ni watundu mnooo huwezi kuwameza kirahisi, ndio maana nimewafananisha na msumari wenye kutu. Hawa watu ni wahuni, huwezi kuwaua kirahisi. Maslahi ya Chadema na CCM yabaki kwanza chini, ila ya Tanzania yetu yawekwe mbele.

Hongera Samia na Mbowe.
FB_IMG_1677688856429.jpg
JamiiForums1267461471_387x387.jpg
 
Back
Top Bottom