CHADEMA inahitaji tume huru ndani ya Chama kabla ya kudai tume huru ya Taifa ya Uchaguzi

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,872
Nimeshuhudia na kushiriki chaguzi nyingi ndani ya Chadema na ndani ya CCM,chaguzi nyingi ndani ya vyama vyetu zinavunja katiba za vyama hivyo kwa makusudi kabisa,wasimamizi wa chaguzi hizo kwa kuwa wanakuwa na mamlaka ya nafasi za uongozi kutoka ngazi za juu,hutumia mwanya huo kufanya kadri watakavyo wao kinyume kabisa na maelekezo ya katiba za vyama hivyo,hivyo basi kabla ya kudai tume huru ya Taifa ya uchaguzi tuanze na chaguzi huru kwenye vyama vyeti vya siasa,kwa maana uimara wa chama cha siasa unaanzia kwenye mifumo ya uendeshaji wa shughuli zake za ndani,na hivi ndivyo viashiria vinavyotazamwa na Umma.

Kwa maoni yangu Bavicha yenye mwendelezo kwa Chaso-Chadema student organization na Uvccm zimedhoofika na kukosa uelekeo na misingi imara baada ya kuathiriwa zaidi na mfumo huu wa chaguzi za michongo maarufu kama connection toka kwa walio juu, maelekezo ya viongozi wa juu dhidi ya kile kinachoitwa kupanga safu za watu wanaowataka kwenye nafasi za chini,waliosoma Cuba wanaita michongo ama connection za uongozi,ukitazama vyema rufaa nyingi na malalamiki ya wagombea kwenye chaguzi nyingi,utagundua kuwa kumbe mambo si shwari ndani ya chaguzi za vyama vyetu hususani CCM na Chadema,tofauti kabisa na tulivyokuwa tunahisi kama mambo ni shwari kiasi hicho.

Nianze kwa kuzungumzia ombwe la michakato ya chaguzi za ndani za vyama vyetu,kwa ufupi nikianza taasisi za awali za vyama yaani Uvccm na Bavicha,taasisi hizi zimekuwa mateka kwa ombwe la vyeo toka kwa viongozi wa juu,vijana ndani ya taasisi hizo wanawaza matumbo yao badala ya kuwaza kesho ya vijana wa Tanzania,baadhi ya vijana toka kwenye taasisi hizo hivi leo wanaitwa Chawa na kesho watakuwa viroboto,huu ni unyanyasaji kwa vijana kuwaita chawa wenu,hivi ninyi viongozi mliokuwa juu,je mlinyanyaswa hivi na Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!??? Taasisi za vijana ndani ya chama haziwezi tena kutembea zenyewe,zimekuwa mateka kwa sababu ya viongozi waliopatikana kama si kwa pesa basi toka kwenye chaguzi zenye maagizo toka juu,

Taasisi hizi za Bavicha na Uvccm ni sauti za wasio na sauti kwa vijana,lakini kwa sababu ya aina ya mifumo mibovu ya uendeshaji wake ikiwemo chaguzi zake kuhodhiwa na wenye maguvu ya kifedha,sasa taasisi hizo zinapoteza muelekeo wake wa mwanzo,Katiba ya Chadema ibara ya 6.3.1(c) inasema mshindi atatangazwa baada ya kupata 50% ya kura zote halali zilizopigwa,kama mshindi wa kwanza kapata 44% kwa kura 136 na wa pili 41% kwa kura 126 basi chaguzi hii ilipaswa kurudiwa Ili kutimiza matakwa ya Katiba ya Chadema inayosema mshindi atatangazwa baada ya kupata 50% ya kura zote halali zilizopigwa,lakini chama kikatangaza mshindi ni yule aliyepata 44%,hapa katiba ilivunjwa.

Kuna wakati niligombea nafasi fulani Uviccm,niliambiwa nilipie nauli za kwenda kuwachukua wajumbe ili waje ukumbini kupiga kura,nililipia Eicher wakaja ukumbini na kweli nilishinda,lakini nilipotaka kugombea nafasi nyingine ya juu zaidi niligonga mwamba niliambiwa nimevuka miaka 35 sistahili kuwa katika nafasi hiyo kwenye taasisi ya vijana,niende jumuiya ya wazazi,wakati huo huo kuna watu wamenizidi umri wapo kwenye jumuiya hiyo hiyo ya vijana ila hawaguswi,nikaachana nalo,mara nyingine nikaenda kugombea Ujumbe wa halmashauri kuu wilaya,sera zangu za kiuchumi ili kukiwezesha chama kupata mapato zikakataliwa,nikashangaa mgombea Uenyekiti wa Wilaya hiyo,akijinadi yeye ni yatima apewe nafasi hiyo,na akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Wilaya hiyo.

Mfano mwingine,binafsi niliwahi kugombea nafasi fulani ya CCM Jimbo fulani wakati wa kupiga kura lililetwa jina la mwenzangu kupigiwa kura,jina langu halipo,kila aliyepata karatasi ya kupiga kura jina langu halipo kumbe mchapishaji alichapisha jina moja kwa makusudi kabisa,hapa unaweza kujiuliza huyu mchapishaji alipewa hela afanye hivyo ama maelekezo toka juu,hiyo imekuwa tabia ya siasa za Watanzania,kwa kifupi maadili yetu yameporomoka sana,hatupo kwenye chama kimoja lakini jina linaletwa moja,hapa tukidai tume huru wakati sisi ndani ya chama hatupo huru,je tutafanikiwa!? Tunahitaji sana tume huru lakini kwanza chaguzi zetu ndani ya chama zinapaswa kuwa huru,kupata viongozi ambao wananchi wanaowataka na si viongozi wanajiweka wenyewe madarakani kwa danganya danganya toto.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es salaam,
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Tume huru ndani ya chadema ni kama usiku wa giza,imagine wafuatua ndio wagombe wa kudumu kwenye nafasi walizo nazo;
1:Mzee Mbowe
2:Lema
3:Wenje
4:Sugu
5:Heche
6Lissu
7: Mnyika
8: Mrema
10:Msigwa
 
Kichwa Cha habari ni cdm, lakini ukiingia ndani ni uhuni wa ccm! Au ndio mbinu siku hizi, ukitaka watu wasome bandiko lako inabidi uwataje cdm!
 
Back
Top Bottom