G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,883
1. Aliyestahili kumpatia taarifa Makamo wa Rais juu ya kifo cha Rais Magufuli ni daktari wa Rais.
2. CDF Mabeyo alikuwa mkuu wa majeshi ndiyo, yeye pamoja na viongozi wengine wa vyombo vya usalama walitakiwa pia kupatiwa taarifa na Makamo wa Rais (Baada ya yeye kuwa mtu wa kwanza kabisa kufahamishwa) ili kuhakikisha tu usalama wa nchi upo vizuri.
3. Makamo wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais inaendeleaje.
4. CDF anachukua majukumu ya kuwa msaidizi mkuu wa Rais na mtoa taarifa kwa Makamo kuwa Rais amefariki (Kosa kubwa) mbaya zaidi Makamo wa Rais anakuwa mtu wa nne kuambiwa baada ya Waziri mkuu, CS na Taasisi ya kiswahili (Baada ya kujadili mpaka cheo cha Amiri jeshi mkuu)
Kosa ni la nani? Hayati Magufuli kujiundia kikundi chake cha siri kwa mambo yao huku wakimuondoa Makamo? Wasaidizi wake wakati Rais ni mgonjwa? Makamo wa Rais yupo Tanga anaongea kawaida tu huku Rais yupo kitandani akipigania uhai na wala hajulishwi hadi umauti tena masaa manne mbele baada ya mijadala ambayo kimsingi watu hawaijui katiba. Inafikirisha.
Sishangai kuona daktari binafsi wa hayati Rais Magufuli Prof. Mabula Mchembe kupotea ulingoni baada ya Samia kuwa Rais? Hivi yuko wapi huyu mtu?