Masanilo
Platinum Member
- Oct 2, 2007
- 22,286
- 4,520
WanaJF,
Siungi Mkono moja kwa moja alichoongea Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mh.Lukuvi Bungeni jioni hii.
Kwanza,Wametoa tuhuma hizi wakati Zitto akiwa hayupo ndani ya Bunge
Pili,Hatuwezi kumuhukumu Zitto moja kwa moja bila kumpa fursa ya kumsikiliza
Napinga tabia hii ya wanaCCM kumdhalilisha Zitto Bungeni na kumnyima fursa ya kujitetea na wengine kuanzisha thread humu.
Tatu,Ni jambo la kusitisha kuwa Chama tawala kina viongozi na makada wanaoweza kuminya haki wazi wazi hasa pale wanapoona kuwa maslahi ya viongozi na wanachama wao yanahatarishwa.Mh.Zitto anayo majina na sio busara kumshambulia kama alivyofanyiwa ili tu kuwanusuru wanasiasa na makada wa CCM waliolimbikiza fedha nje
Nne,Naomba Wanachama na viongozi wa CCM,Wabunge na Viongozi wa Bunge waige mfano bora wa CHADEMA kwa kumpa nafasi ya kujitetea.Natural justice ni jambo la msingi.Tuimarishe misingi ya uwazi katika suala linalohusu maslahi ya nchi.
Namshauri pia Mh.Zitto aweka wazi suala hili hasa suala la kutaja majina ya wamiliki na kama hawezi anaweza kumpatia majina haya Mhe.Lema ayataje.
Kama task Force ya Bunge iliweza kuvujisha majina ya waliochunguzwa,ni kitu gani kinamshinda yeye kuvujisha majina kwa Lema ambaye yupo tayari kutaja bila woga?
Tumpe nafasi badala ya kumzomea na kumshutumu jamani.