Mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2005, kila kukicha tunasikia CCM wakiongelea ni nani atakayemrithi Kikwete. Kambi nyingi zimetajwa na baadhi ya wanaCCM wameshajipambanua wako kambi ipi. Hata hivyo wakati wakihangaika kumpata mrithi wa Kikwete, Nchi wananchi wengi wanazidi kuwa maskini, majangili na wauza unga wanazidi kutamba. Je CCM hawana mipango mingine zaidi ya kuwaza nani ataingia ikulu?