Burning issue: Mchakato wa uagizwaji wa mafuta nchini-petroleum bulk procurement system

Mugabe Tz

Senior Member
Apr 6, 2016
196
215
Habari za mchana huu wana JF wenzangu...........................Poleni na harakati za kufanya mkono uende kinywani

Kwa faida ya wengi, naomba mods msiuunganishe uzi huu na nyuzi nyingine kutokana na unyeti na umahsusi wa mada tajwa humu.

Naomba kwa yoyote anayefahamu kwa kina kuhusu mchakato mzima wa uagizaji na ununuzi wa nishati ya mafuta atufahamishe kwa faida ya Watanzania wote ili tunapoona bei kwenye mabango ya vituo vya mafuta tuweze kuelewa. Naomba maelezo hayo yaguse maeneo haya mahususi;

i. Jinsi mchakato mzima unavyofanya kazi, toka kuagiza mpaka kumfikia mlaji wa mwisho
ii. Historia ya mfumo huu, je kama Taifa tuna muda gani tumekuwa tukiutumia, na hapo kabla tulitumia mfumo upi
iii. Je, nchi nyingine pia zinatumia mfumo kama wetu katika kuagiza mafuta (Mfano; Zambia, Malawi, Kenya)
iv. Kama zinatumia mifumo mingine, ufanisi wa mfumo wetu uko vipi ukilinganisha na hii mifumo mingine
v. Taratibu ambazo Taasisi ya EWURA wanafuata kabla ya kutangaza bei mpya kila mwezi, bei hizi huidhinishwa na nani kama mtu wa mwisho kabla hazijatangazwa kwa Umma
vi. Kuna uwezekano wa mfumo huu kuingiliwa na watendaji kwa maslahi yao binafsi?

Ufafanuzi huu wa kina utatusaidia kuelewa jambo hili kwa kina na kutuwezesha kuchanganua maneno mengi yanayosemwa kuhusu jambo hili.

Karibuni tupate maarifa

Natanguliza shukrani zangu za dhati

🙏🙏🙏
 
Katiba mpya ndiyo suluhisho....

Hapa tungekuwa nayo viongozi wangewajibika zaidi kuliko kusingizia vita ya ukraine na urusi..

Sote tulikuwa tunajua vita itapandisha vitu hivyo.viongozi hawana haja ya kutuambia, walichopaswa kutuambia ni wamechukua hatua gani kukabiliana na hili jambo.


Screenshot_20220504-122747.jpg
 
Back
Top Bottom