JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Kesi hiyo ambayo inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Amiri Msumi ambaye ametupilia mbali baada ya kuona mahakama hiyo haikuona haja ya kuendelea kushikilia pingamizi hilo kutokana na kukosa mashiko kwa mujibu wa sheria.
Hakimu Mkazi Mkuu, Amiri Msumi alisema baada ya mahakama kupitia nyaraka zilizokuwepo mahakamani na kuona kilichokuwa kinapingwa mdaiwa (Mwakinyo) ni tarehe ya uthibitisho wa madai ya Paf ambayo mahakama iliona imejazwa kwa usahihi kuwa ni tarehe 11.10.2023.
Hivyo, mahakama hiyo imesema pingamizi halina mashiko kwa kuwa nyaraka inayoaminiwa ya kwanza ni iliyopo mahakamani na imejazwa vizuri kwa mujibu wa sheria, hivyo mahakama imeona haina haja ya kushikilia pingamizi hilo kwa kulitupilia mbali.
Mahakama imetoa amri kwa kuwa kesi iendelee kwa kongamano la awali (fist pre trial conference' ambayo imepangwa kusikilizwa Aprili 23, 2024 Saa Sita Mchana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Amri Msumi.
Katika kesi hiyo, Kampuni ya PAF Promotion inawakilishwa na wakili msomi, Herry Kauki wakati Hassan Mwakinyo kwa upande wa mdaiwa akiwakilishwa wakili msomi, Azad Athumani.
Chanzo: boxinghubtz
Pia soma:
- Hatimaye wakili wa Mwakinyo kafika mahakamani leo
- Kampuni ya PAF Promotion yampeleka Mahakamani Mwakinyo, yamdai fidia ya mamilioni