Bi Bernadette Olowo

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
351
853
Pichani ni mwanamke wa kwanza duniani kuwa balozi ndani ya Vatican city, alikuwa balozi mdogo (Ambassador Extraordinary & Plenipotentiary to the Holy See at the Vatican) kutokea Uganda.

Idi Amin alikiwa mtu na nusu, alivunja mila huko Vatican, na kuweka historia kwa kumteua na kumtuma mwanadiplomasia wa kwanza wa kike Vatican.

Ngoja niweke sawa kidogo...

Kabla ya mwaka 1975, Nchi ya Vatican city (Holy See) ilikuwa aijawahi kupokea balozi yoyote wa jinsia ya kike, huu ndio ulikuwa utamaduni na mila ya Vatican (Plenipotentiary to the Holy See), zipo sababu nyingi juu ya mila hii, ntaeleza hilo siku za usoni.

Sasa basi...

Tarehe 23 January 1975 Idi Amin alimteua Bi Bernadette Olowo, muhafidhina wa Kikatoliki na muumini kindakindaki wa kanisa la Katoliki, kuwa Balozi Mdogo huko Vatican city.

Amin aliandika historia hiyo Januari 23, 1975, kwa kumteua mwanamke wa kwanza ambae pia Vatican ilimtambua kama Balozi Mdogo.

Bi Bernadette Olowo ndio balozi wa Kwanza wa jinsia ya kike huko Vatican city katika kipindi cha miaka 900, yani kwa zaidi ya miaka 900 Vatican aikuwahi kupokea wala kumkubali balozi yoyote yule wa kike.

Ndimi Comred Mbwana Allyamtu CMCA.
FB_IMG_1668277753281.jpg
View attachment 2415294
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom