Bei ya luku ishuke, viwanda vifufuliwe, wananchi wapikie majiko ya umeme kuzuia uharibifu wa mazingira

TANESCO nao wasanii...Kijijini nguzo moja ni Laki 5. na kuunganisha ni 27000

Yaani ni miti aina gani?
Nguzo Huwa zinanunuliwa miti yake mafinga, zinapigwa stika ya south Afrika, tanesco wanazinunua Kwa Bei ya sa, pesa zinaingia mifukoni mwa wakubwa.

Wizi na RUSHWA ndo chanzo Cha gharama kubwa ya uendeshaji na HASARA tanesco tunaongezewa Bei ya luku.
 
Bei ya umeme ishuke Ili kufufua viwanda na kuchangamsha Uchumi wa wananchi.
 
Salaam, Shalom.

Samahani Kwa waliozaliwa 2000+, Miaka ya 90 kurudi nyuma, yalikuwepo majiko ya umeme katika nyumba nyingi za watumishi wa umma, mapolisi, mahakimu, bankers, watoza ushauri, matajiri nk nk.

Matumizi ya majiko ya kutumia umeme, yalisaidia kupunguza matumizi ya mkaa, hivyo kuzuia uharibifu mkubwa wa mazingira na kupunguza matumizi ya mkaa na Kuni.

Hivi sasa, kaya nyingi zinatumika majiko ya Kuni na mkaa Kwa wingi,gesi kidogo.

Kwa kuwa nchi yetu imekopa matrilioni kujenga BWAWA la JNHP, na Kwa kuwa walipaji wa deni Hilo ni sisi wananchi, na Kwa kuwa majiko ya umeme Yana faida zaidi kimazingira, na Kwa kuwa Bei kubwa za luku ni chanzo kikubwa Cha kutotumika majiko ya umeme nchini Kwa wananchi wa kipato Cha chini,

Na Kwa kuwa, mradi wa REA kuunganisha vijiji Kwa huduma ya umeme umewafikia wengi, uwezekano wa kutumia umeme kupikia ni mkubwa zaidi Hadi vijijini.

Ninashauri Bei za luku zishushwe Ili wananchi waongeze matumizi ya umeme Kwa kupikia ili kuboresha na kutunza mazingira.

Kushushwa Bei za luku Kuna faida ZIFUATAZO;

1. Matumizi ya umeme yataongezeka na mapato pia yataongezeka hivyo kulisaidia shirika kujiendesha Kwa faida..

2. Serikali itaongeza ukusanyaji wa mapato Kwa ajili ya kulipa mikopo iliyotumika kujenga BWAWA la JNHP.

3. Matumizi makubwa ya umeme wa kupikia majumbani, itaongeza matumizi ya mitambo ya kufua umeme, hivyo kuondoa hatari ya kuchakaa na kiharibika mitambo Kwa kuzimwa mara Kwa mara.

4. Kupunguza gharama za umeme Kwa wananchi kutachagiza viwanda vidogo vidogo , viwanda vya kati na vikubwa kuoperate Kwa faida kubwa hivyo kuinuka Kwa kipato na mxunguko wa pesa, Uchumi utakua na export zitaongezeka.

5. Kupunguza gharama za umeme kutusaidia kuondoa mafuriko Kwa wakazi vijiji vinavyopakana na BWAWA la JNHP Kwa kuwa mashine za kuzalisha umeme zitatumika ipasavyo hivyo kupunguza zoezi la kumfungulia maji ya BWAWA Hilo.

USHAURI:

Ikiwa Kwa sasa ukinunua umeme wa sh 5,000 unapata unit 14,

Tafsiri hapo ni kuwa, 1unit =sh 357.

Bei ishuke kuwa 1unit =sh 10.

Ili Ukiwa na sh 5000 upate Unit 500.

Hapo itawezekana kupikia majiko ya umeme Hadi huko bush Kwa bibi zetu.

HITIMISHO:

Kupungua Kwa gharama za umeme wa luku Kuna faida kubwa kiuchumi, Kijamii, kisiasa, kiafya, ninashauri Serikali yangu kuacha mawazo ya kuuza umeme nje ya Nchi, umeme upunguzwe Bei kufufua viwanda vidogo vidogo vya kati na vikubwa tupate faida za kiuchumi.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Amen

Karibuni🙏
Taarifa: Wingi wa jiko ni meko na siyo majiko. Omba mods wakurekebishie heading.
 
Taarifa: Wingi wa jiko ni meko na siyo majiko. Omba mods wakurekebishie heading.
Loh, sikulijua hili, ngoja nipitie kamusi,

Hata hivyo NENO " Meko ya Umeme" wengi hawaujui msamiati huo.

Acha ibaki hivyo hivyo imeeleweka.

Ahsante Kwa ufafanuzi, na karibu utoe michango wako.🙏
 
Chama cha Ma-vampire kimetugeuza wananchi Mazombi
Wanataka Wananchi walipe Kodi ilhali Bei za umeme ziko juu,

Sasa Bei ingepungua, viwanda vidogo vidogo vingeongezeka sababu ya nafuu ya Bei ya nishati!!

Hawa sijui uchumi wamesomea wapo🤔
 
Back
Top Bottom