Barua ya wazi kwa waziri Doroth Gwajima

MwanaWA Ebrania

JF-Expert Member
Oct 6, 2017
940
1,139
Barua ya wazi kwa waziri, Daktari Dorothy Gwajima.

==========

April 12, kila mwaka ni siku ya mtoto anayeishi mtaani duniani.

Tanzania ni moja ya taifa linaloadhimisha siku hii.

Watoto wa mitaani usababishwa na tatizo la malezi ktk ngazi ya familia.

Tunapoazimisha siku hii, naomba niandike ujumbe mfupi kwa jamii na Serikali yangu hasa kwa mhe: waziri maendeleo ya jamii, daktari Dorothy Gwajima.

Nikupongeze kwa kuaminiwa na mheshimiwa Rais wetu mpendwa kukuamini uongoze wizara hii nyeti inayojenga msingi imara wa jamii na taifa letu.

Nikiwa kama kijana muhanga niliyeathirika na maisha ya kuishi mitaani, na sasa ninafanya kazi kama mdau na mpambanaji wa haki za watoto ktk kipengele cha kutoa elimu ya malezi bora ili kupunguza ongezeko la watoto waishio mitaani.

Naona kunajitihada za makusudi zinafanywa za kutengeneza ongezeko kubwa zaidi la watoto waishio mitaani. Aidha kwa kujua ama kutokujua.

Tangu wizara hii imeundwa, kuna kampeni mbalimbali zinafanywa na vijana me & ke.

Binafsi, mwanzoni nilitegemea kampeni hizi zitakuwa chachu ya kupunguza ama kuondoa kabisa ukatili pamoja ongezeko la watoto hao wa mitaani.

Kumbe ni tofauti, kampeini hizi nyingi zimekuwa sasa zinazalisha ongezeko la ukatili na watoto waishio mitaani, serikali hisipochukua hatua ya haraka miaka michache hijayo tutashuhudia wimbi kubwa zaidi la watoto waishio mitaani.

Sababu kubwa ni hizi:

1- Kuna wimbi kubwa la wasichana wanatumika kujiuza, kwa style ya kuomba omba kupitia kampeni hizi, dada zetu hawa

Hawafanyi hivyo kwa kupenda, ila wanafanya ili wapate kitu chochote cha kula, vouchers za simu, pamoja na nauli ya kwenda na kurudi kesho.

Kampeni hizi zimekuwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza watoto wasio na baba kama kuku wa mayai.

Yenyewe wanajisifu kabisa bora niwe single mother.

2- Ndoa nyingi za hao vijana wanaoshiriki kwenye hizi kampeini zinavunjika kwa kasi,

Hazivunjiki kwa sababu wanapenda, ila kwa sababu wengi wao hawana chakula kisa tu vijana hao wameacha majukumu yao ya kujitafutia mkate wa siku, wao wanaenda kwenye kampeini ili wapige picha na waziri ama na viongozi wa hizo kampeini, ambazo mwisho wa siku wanajikuta jioni inawakuta hawajaingiza chochote kitu, na wengine hata nauli ya kurudi nyumbani hawana,

Wanaanza kuomba omba.

Kumbuka hawajala tangu asubuhi.

3- Kampeini hizi zinaenda kutengeneza ongezeko la vijana wetu kuwa mashoga, matapeli na kulelewa na mishangazi.

Sababu wengi wa vijana hao hawataki kufanya kazi ngumu ya kujitafutia kipato.

Wengi wao wanaamini siku moja waziri atawaka kwenye nafasi fulani huko wizarani.

Hivyo vijana wanajikuta wanakazi ya kuomba pesa za nauli na kula kila siku kwa wanaume wenzao, ambao mwisho wa siku ujikuta wameingia kwenye mfumo wa kutumika miili yao kwenye matendo maovu.

Mwisho wa siku jamii yetu inatoa lawama nyingi za kilio kwa kuichukia serikali yetu.

Hizi kampeini zote zinazojiita za kutokomeza ukatili, ndani yake zinaongozwa na watu wenye fikra dumavu za afya ya akili.

Watu hao hawataki kupewa fikra chanya.

Mfano mdogo: mtu mwenye fikra dumavu, anaanzaje kutoa hamasa za kumshawishi mtu anayefanya ukatili aache?

Nikiwa miongoni mwa vijana waliozunguka kwenye ziara zako nyingi bila kula kuanzia asubuhi - jioni

Bila nauli.

Nimekuwa nikiwa nikitoa vincent vyangu vya akiba kusaidia vijana hao wazalendo ili wapate nauli na kula kila wakati.

Mwisho wa siku vijana hao wanataka kunipa fadhila za miili yao

Naandika hii barua naumia toka ndani

Vip nisingeishi mitaani na kuzijua shida

Nami ningekuwa miongoni mwa vijana wajinga

Vipi ningekuwa miongoni mwa binadamu wenye fikra katili

=====

Mhe waziri,

Japo ninamengi,

Naomba niishie hapa.

=======

#"Tuwajibike" "Belonging".

#Tanzania salama bila ukatili:inawezekana.

By: James Yustar.

FB_IMG_1699272118265.jpg
 
Back
Top Bottom