SI KWELI Barua ya NECTA kuratibu zoezi la Kurekebisha Makosa ya majina kwenye vyeti vya Mwaka 2000-2023 kwa Malipo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Nimeona barua inasambaa Mtandaoni ikisema NECTA inaratibu zoezi la Kurekebisha Makosa ya majina kwenye vyeti vya Mwaka 2000-2023 kwa Malipo.

Barua hii inanipa mashaka sana, JamiiCheck nisaidieni kuhakiki.

UZUSHI BARUA.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na barua inayosambaa mtandaoni ikisema Baraza la Mitihani la Tanzania linawajulisha watu wote utaratibu wa kufanya marekebisho ya majina kwa walio na utofauti wa Majina kwenye Vyeti vya Elimu na NIDA ili kuondoa mkanganyiko wa taarifa wanapo omba ajira kwenye mfumo na kwamba Marekebisho haya yana wahusu walio maliza kidato cha nne au sita kwa mwaka 2000-2023.

Kwa mujibu wa barua hii, gharama za marekebisho ya majina kwenye vyeti vya NECTA au NACTE ni Tsh. 47,850, harama za marekebisho kwa vyeti vya taaluma kwa ngazi ya Cheti, Diploma na Shahada ni Tsh. 65,750 na wote wanaohitaji kufanyiwa marekebisho wanasisitizwa kuhakikisha wanatuma viambata Cheti cha kuzaliwa, Namba ya NIDA au Kitambulisho na Cheti au Vyeti vinvyo hitajika kufanyiwa Marekebisho viambata vyote vitumwe kwa barua pepe vvet@necta.go.tz au WhatsApp 0615 498 952 kwa taratibu za marekebisho.

Ukweli wa Barua hii
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa barua hii haijatolewa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kama inavyodaiwa.

Taarifa hii inakinzana na utaratibu rasmi uliobainishwa kwenye tovuti rasmi ya NECTA ambapo mtu anayetaka kubadili vyeti hupaswa kulipia Tsh. 35,000 tu na siyo Tsh. 47,850 au 65,750 kama ilivyooneshwa kwenye barua hii.

Maombi ya kubadili majina hushughulikiwa na shule, Mkuu wa shule/Mwalimu Mkuu kwa kujaza fomu ya marekebisho au ‘Query Circular Form’ inayobainisha kosa lililofanyika katika jina na jina sahihi linavyotakiwa kuandikwa au yanapaswa kujazwa moja kwa moja kwenye tovuti ya Baraza na siyo kutuma kwa njia ya WhatsApp au email kama inavyodaiwa kwenye barua hii.

Aidha, Aprili 12, 2024, NECTA ilikanusha barua hii kupitia Mtandao wa X kwa kuiwekea alama ya FAKE NEWS.

Baadhi ya mambo yanayoweza kutumika pia kuonesha jinsi barua hii ilivyo ya kughushi ni kukosewa kwa Jina la NECTA kwenye point ya 2 ambapo barua imendika NECTAR pamoja na kuweka namba ya Mtandao wa WhatsApp kama njia rasmi ya mawasiliano ya ofisi ya Serikali, jambo ambalo siyo sahihi.
Cheti changu kilikosewa jina. Nimepoteza deals nyingi kwa kuambiwa nimeghushi cheti.

Mbaya zaidi nilikuja gundua hilo wakati natafuta namba ya NIDA ndio kugundua jina limekosewa kwenye cheti. Niliambiwa nipeleke nakala ya cheti cha kuzaliwa kisicho na makosa. Cheti cha kuzaliwa nimekipata ukubwani nacho kina majina halisi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom