JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,323
- 5,493
Hali ya Barabara Africana njia ya kuanzia kwa "Kwa Barikiwe" kuelekea Kinzudi ni mbaya mamlaka zitusaidie hata kukwangua matope maana ni kero kwelikweli sio kwa watembea kwa miguu bali hata wenye magari, Bajaji, pikipiki na Watumiaji wote tunapata tabu.
Kero hii imechangiwa na waliomwaga udongo wakituaminisha ni kifusi, lakini ukweli usemwe, kilichowekwa sio kifusi cha kuweka kwenye barabara ya aina hiyo, kile ni kifusi cha gadeni (bustani) maana udongo mtupu.
Kifusi hicho kimemwagwa kwenye kipindi hiki cha mvua, najiuliza wahusika walikuwa wanalenga nini, ni kweli barabara hiyo ilikuwa na changamoto ya mashimo lakini ndio watuwekee kifusi cha aina hiyo? Hivi Mbunge na wasaidizi wake ikiwemo Diwani hawalioni hili jamani!
Kuna ambao kabisa tumepaki magari, maana watu tokea juzi magari yanaharibika yakipita kwenye njia hiyo, Wafanyabiashara wa maeneo ya juu Kinzudi wanapata changamoto kupata mizigo, Wanafunzi wetu hasa wanaosoma Shule ya Msingi Kinzudi na wengine wanapata tabu, bodaboda na Bajaji wameanza kupandisha bei wengine wanasitisha ruti badala yake wanashusha abiria kwa Barikiwe Center kutokana na ubovu wa barabara hiyo, jambo ambalo ni kero.
Hali hii ikiendelea hivi mambo yatazidi kuwa mabaya, hatua zichukuliwe, Viongozi wawajibike kutuwezesha kuwa na mazingira Bora ya kupita.