Baadhi ya Waafrika waliopo kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi duniani

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
87
103
Kwa mujibu wa jarida la Times limetoa orodha ya watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani kwa mwaka 2024 tarehe 17, Aprili 2024. Orodha hii imejumuisha watu wanaoshughulika na sekta mbalimbali kama biashara , Sanaa, michezo, muziki na nyingine nyingi.

Wafahamu baadhi ya waafrika waliopo kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi duniani kulingana na Jarida la Times

1. Burna Boy- Nigeria

Ameweza kuwakilisha muziki wa Afrika kimataifa. Pia, amekuwa mwanamuziki wa kwanza kutoka Afrika kutumbuiza kwenye tuzo za Grammy mwaka 2024.

2. Rais William Ruto- Kenya

Ameonesha ushawishi kwenye kushughulikia masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa na kubaini changamoto za hali ya hewa zinazohitaji kushughulikiwa nchini Kenya.

3. Siya Kolisi- Afrika Kusini

Ni nahodha wa timu ya taifa ya rugby ya Afrika Kusini. Jitihada zake zimeonekana kipindi cha COVID 19 kwa kulipa taifa hilo tumaini baada ya kushinda mashindano ya kitaifa ya mchezo wa Rugby Afrika Kusini.
 
Back
Top Bottom