Baadhi ya mipango ya serikali inayo-trigger 'emergency alarm' na inayotakiwa kutupiwa jicho na jamii nzima

Escrowseal1

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
4,445
4,236
Si aibu kusema kuwa watanzania tuko vulnerable linapokuja suala la ufisadi barani Afrika hasa kwa experience tunayopata awamu zote tunazopitia.

Tunavyoenda ni ukweli ulio wazi kuwa hiki kipindi ni volatile na tunahitaji jamii nzima kuwa so sensitive na mipango ya serikali. Binafsi na nadhani baadhi washapata wake up call na baadhi ya mipango ya serikali inayoweza kutu rejuvenate kwenye experience.

1. Mipango ya kubinafsisha bandari. Kwa uwekezaji uliokwishafanywa na serikali ukisaidiwa na WB katika bandari ya Dar es salaam,kilichokuwa kimebaki serikali ilitakiwa ipambane kusharpen vijana wetu ili tupambane kupata efficiency badara ya kuvutia uwekezaji sehemu ambayo ishawekezwa na mvutia wawekezaji. Hii habari inafikirisha sana tutakuja kuambizani huko mbele.

2. Wawekezaji wanaotarajia kujenga barabara zetu. Tumezoa kukopa na kujenga barabara zetu kwa mikopo na kulipa madeni.

Hii habari imesikika hata kwenye miradi ya reli kuwa ma capitalist wanaweza kuja kutujengea vipande vya reli na kurudisha gharama zao.

Sina uhakika how it works especially under ccm Gorvernment ila haya mambo yote mapya hasa yanayoletwa na serikali ya ccm yanatakiwa ku trigger alarm .hasa kwa experience tulokuwa nayo na hii serikali.

3. Uwekezaji kwenye miradi inayoendelea kama mwendo kasi. Once niliwahi kusikia kuwa ufaransa imevutiwa kuwekeza kwenye mabasi ya mwendokasi. Huu ni mradi tuliokuwa nao uzoefu wa almost 10 years hivi research and development yetu kwenye miradi huwa inafanya nini mpaka tu attract investors kwenye miradi inayo run. Hizi nchi kama ufaransa for hundred of years wako far away hadi kutengeneza ma airbus ni nini kinatufanya tuwavutie kwenye miradi iliyo take off badala ya ku improve wenyewe.

4. Kama si pressure ya mashirika ya nje basi serikali ya awamu hii inaamini katika private sector kuliko habari nyingine. Yes tunahitaji hii sector ikue ila binafsi nadhani nayo inahitaji kuwa nurtured ikue yenyewe hasa kwa miradi mipya na si ku give away roho za nchi na miradi yetu ya ki mkakati. Mara nyingi ukiwa unapata kongole kutoka kwa mashirika fulani fulani hasa kwenye bara letu ,jifungie ndani ujikague maana kama hujaangukia pua paji la uso utakuwa huna.

Hiyo ni baadhi tu na ni ruksa kuongeza. Itoshe kusema kwa kuwa si siri watanzania tuko vulnerable hasa kutokana na background yetu. Ni collective effort tunayopaswa kuwa nayo hasa tunapoona mambo ndivyo sivyo.

Ilitusaidia kwenye ndege zilizoanza kutua kwenye mbuga na hata kwenye bandari ya bagamoyo. Ni vema tunapoona mambo yanayokuja ndivyo sivyo tukasimama imara kwani mwl alipata kusema matajiri wanaungana iweje sisi mafukara.

Pamoja tutashinda.
 
Umekiri kuwa awamu zote ufisadi umekuwa tatizo - sahihi kabisa.

Na kama ilivyo kwa ugonjwa au tatizo lolote lisiposhughulikiwa kikamilifu basi hukomaa na kuzidi kuwa kubwa na baya, ndiyo hali ya nchi yetu.

Chanzo ni utawala mbovu ulioleta mfumo mbovu na katiba mbovu. Hatujawahi kuwa serious kushughulikia ufisadi na rushwa. Wala hakuna ushahidi wa hilo.

Wazungu na Wachina wanatumia udhaifu huo kujinuifaisha. Dunia haina mjomba wala shangazi wa kutusaidia, ni sisi wenyewe tu.
 
Tunapongeza uthubutu katika miradi mikubwa,Ila tunapaswa kuwa na mifumo thabiti ya kupembua vipaumbele vya nchi kwa maslahi mapana ya Taifa kwa miaka 25 mpaka 50 ijayo.

Mipango na bajeti zenye kujenga legacy ya viongozi badala ya taifa hazitufai..Utaalaamu na uzalendo vipewe nafasi zaidi kwa kutambua nchi yetu bado ni maskini sana na udhati wa wanasiasa kunasua wananchi toka ktk dimbwi la umasikini wa fikra,kipato,elimu na uchumi.
 
Back
Top Bottom