tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 22,325
- 19,109
Baada ya TEC kuukataa mkataba wa DPW hadharani bila kumumunya maneno, sasa tunasubiri tamko la BAKWATA nao tusikie watasema nini. Ni matumaini yangu kwamba BAKWATA watafuata nyanyo za TEC kwa kuukataa mkataba wa DPW bila kupepesa macho.
Aidha, inawezekana BAKWATA wakaukubali mkataba na endapo watafanya hivyo basi watakuwa na sababu za msingi. Au wanaweza kuukubali na kutoa maoni kuhusu kuboreshwa vipengele vyenye utata, hasa vile vinavyohusu muda wa mkataba na vinavyobagaza mamlaka ya nchi (sovereignty).
Kimsingi ni vigumu kubashiri nini BAKWATA watasema lakini kwa kuwa bado hawajatoa tamko hadharani, ngoja tusubiri tuone watakuja na tamko zito au jepesi kiasi gani. Waswahili wanasema 'usiusemee moyo' au 'usiandikie mate wakati wino upo'. Kwa maana hiyo, hebu tuvute subira kidogo tusubiri kusikia BAKWATA watakuja na tamko la aina gani. Wakati ukifika wataanika kila kitu hadharani. Subra yavuta kheri.