#COVID19 Baada ya Kukubali Chanjo, na Rais Samia Kuchanja, Kiongozi yeyote anayepinga Chanjo hadharani ni 'Insubordination' na usaliti

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,657
113,883
Wanabodi,

Hii ni mada mwendelezo wa mada hii ya wiki iliyopita

Screen Shot 2021-08-05 at 4.27.16 PM.png

Kwa vile zoezi la chanjo ya Uviko linaendelea, Kwa Maslahi ya Taifa inaendelea kujikita kwenye chanjo, leo nikiangazia hoja ya uhiari wa Chanjo. Japo chanjo ni hiari, hiari ya chanjo ni hiari ya consent kama ilivyo kwenye mahusiano ya ndoa, ndoa ni hiari, na sio ule uhiari wa choice kama kwenye uchaguzi, mtu uko huru kujiandikisha kupiga kura, au kutokujiandikisha, na hata ukijiandikisha, bado uko huru kupiga kura au kutokupiga kura, hiyo na uhiari wa choice, lakini uhiari wa chanjo ni uhiari wa consent, kama ulivyo uhiari wa kuingia kwenye mahusiano ya ndoa, ukiisha ridhia kuingia kwenye ndoa, uhiari wa ndoa unaishi hapo, kinachofuata ni wajibu, kuihudumia ndoa sasa inakuwa sio hiyari tena, ni wajibu, mwanaume lazima awajibike kumhudumia mkewe, sio hiri ni wajibu, na wanandoa hao wana wajibu wa kuihudumia ndoa, ndia maana kwenye ndoa za kiafrika kuna baadhi ya malalamiko ya wanawake wa kizungu, huku kwetu huwezi kuyasikia. Wenzetu wazungu, hata baada ya kuingia kwenye ndoa, ili mwanandoa kupata huduma za kindoa, lazima aombe tena ruhusa, aridhiwe ndipo akubaliwe, hivyo hiari inaendelezwa hadi kwenye huduma wakati ni wajibu.

Hivyo ndivyo ulivyo uhiari wa kwenye hii chanjo ya Uviko, kwa vile lengo la chanjo ni kinga, kuzuia kuenea kwa uviko, una chanja ili kujikinga wewe na kuwakingi wengine, mtu unapokataa kuchanja, sio tuu unahatarisha maisha yako, bali una hatarisha kuwaambukiza wengine, hii ya kuwakinga wengine sasa sio choice, ni wajibu. Ili kupata chanjo ile hiari ni kwenye kuridhia tuu, yaani ku consent, na sio hiari ya choice kuamua uchanjwe au usichanje, hivyo baada ya nchi kukubali chanjo, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Amiri Jeshi Mkuu, wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mhe Rais Samia Suluhu Hassan Kuchanja, akifuatiwa na viongozi, kitendo hicho japo ni hiari, hiyo ni silent marching order, amri ya kimya kimya, hivyo viongozi wote wa umma, wana wajibu wa kuchanja, sio hiari!. Jee viongozi wetu wote wa umma, wanajua, kuwa baada ya nchi kuibali chanjo na Rais Samia na viongozi wakuu kuchanja, kiongozi yoyote wa umma, anayeipinga chanjo hadharani, kitendo hicho ni Insubordination?. Tunamuomba Mhe Rais Samia, "Please stop this nonsense !"

True Story Yangu na Insubordination.
Mimi nilikuwa mtumishi wa umma pale TBC, enzi hizo TVT, nikiendesha vipindi vya siasa, "Ulingo wa Siasa", tayari nchi yetu ilikuwa ndani ya mfumo wa vyama vingi, hivyo mtu kuwa mtumishi wa umma, hakuna ulazima kuulizwa uko chama gani. Wakati Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, katika vipindi vyangu niliwakaribisha wanasiasa. Kwa vile CCM ndio chama tawala na Tanzania tunaingia chaguzi zote huku CCM ikiwa tayari na uhakika wa ushindi, hivyo nikiwaalika wagombea wa CCM kwenye urais, wanakuwa busy, after all si uhakika wa ushindi upo, ila ukiwaita wapinzani ni fasta.

Baadhi ya watu wakajenga dhana kuwa huyu mwendeshaji wa kipindi, Pasco Mayalla ni pro-oppostion, anawapendelea wapinzani!. Hawajui kuwa ukiwaalika CCM, wanakuwa busy. Nikaenda kupiga kambi Zanzibar, huko nako hali ni ile ile kwenye wagombea urais.

Baada ya uchaguzi, ikafanya tathmini, na wafanya tathmini, ikaonekana Pasco Mayalla ni kama alipendelea upinzani!. Wakatumwa watu kutoka huko walikotumwa, wakaja pale TBC, nikaitwa ofisini kwa Mkurugenzi, nikatambulishwa kwa wageni, na kuulizwa mimi ni chama gani?. Kwanza nilishangaa swali gani hili?!, kwani kuwa mtumishi wa umma, kuna takwa la chama?!. Nikawajibu watu wale ukweli wangu kabisa kuwa mimi Pasco Mayalla sina chama chochote!. Kumbe jibu hilo ni kama kosa!. Mahojiano yakaishia hapo. Baada ya muda, nikaletewa barua ya summary dismissal kwa kosa la insubordination!. Barua ya termination kabla haujakabidhiwa, yule mtu wa despatch anaanzia getini, anapewa FFU wawili wenye silaha, na kuja huku wameshika silaha standby!. Ndipo unakabidhiwa barua, kisha askari hao wanakusindikiza hadi kwenye meza yako. chukua kilicho chako, kabidhi ofisi, kisha unasindikizwa hadi nje ya geti!. Kiukweli nililia!.

Kesho yake nikaenda Utumishi kuuliza hiyo summary dismissal imekaaje, ndipo nikajulishwa kwa mujibu wa utumishi wa umma, ukifukuzwa kazi kwa insubordination, hata kama ni majungu, hakuna popote pa kwenda, you just pack and go!.

Kiongozi wa Umma Kupinga Chanjo Hadharani Sio Tuu ni Usaliti, Bali Pia ni Insubordination!.
Kwenye vita yoyote ya kitaifa, kama ilivyo vita ya Corona, ili kushinda vita, viongozi wote, lazima wasimame pamoja na kuwa kitu kimoja na kuzungumza kwa kauli moja. (must stand as one). Tanzania kama Taifa likiisha kubali Chanjo ya Covid Ndio Maslahi ya Taifa, Viongozi wote wa umma, wanakuwa bind na a collective responsibility clause, they must support, msimamo wa serikali.

Na kama kuna kiongozi yoyote wa umma, hukubaliani na chanjo, hakubaliani na msimamo huo wa serikali, wa kuhimiza Watanzania tuchanje, then kiongozi huyu unapaswa kunyamaza kimya. Kama rais anesema tuchanje, anahimiza Watanzania tujitokeze kwa wingi kwenda kuchanja, sio tuu ili kujikinga sisi wenyewe, bali kuwakinga wengine na kulikinga taifa, kitendo cha kiongozi yoyote wa umma, kujitokeza hadharani, kuwapotosha Watanzania tusichanje, huku ni kwenda kinyume cha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni highest order of insubordination ambayo haipaswi kuvumiliwa au kufumbiwa macho.

Kitendo cha kupingana na msimamo wa serikali wazi wazi ni usaliti, mtu wa aina hii anatakiwa kushughulikiwa haraka iwezekanavyo kama wanavyoshughulikiwa wasaliti wengine wote, na jinsi kosa la insubordination linavyoshughulikiwa na hatua ya kwanza ni kiongozi wa aina hiyo, kuachia ngazi kama mtumishi wa umma.

Kama mtu aliweza kupewa summary dismissal kwa kudhaniwa tuu kuwa sio mwenzetu, jee mtu anayepingana na rais wazi wazi katika jambo lenye maslahi kwa taifa, anaachajwe kuendelea kuipotosha jamii?!. Au Tanzania tuna watu wa aina mbili, the touchables, na untouchables?. Tunakuomba sana Mhe, Presidaa SSH, P'se Stop This Nonsense!.

Wasalaam

Paskali
 
Nimepapenda hapo uliposema "wana wajibu wa kuwalinda wengine" tatizo linakuja huu wajibu utatekelezwa vipi?

Wakati mwingine itabidi utekelezwe kwa lazima, na ukifanya hivyo wajinga watazidi kupata sababu ya kuwadanganya wenzao wasichanjwe sababu zina "matatizo", hili litazidi kurudisha nyuma juhudi za kuwachanja watu.

Time is the best solution hapa kwa mtazamo yangu, naona hofu kuhusu chanjo imeanza kuondoka, watu wanaonekana wakichanjwa na kuendelea na maisha yao kama kawaida.

Hii inasaidia kuwashawishi wengine wakachanjwe na wale wapiga kelele kupinga chanjo naona wataishiwa hoja ndani ya muda mfupi ujao, upinzani wao umeanza kugeuka kama upepo unapita.
 
Nimepapenda hapo uliposema "wana wajibu wa kuwalinda wengine" tatizo linakuja huu wajibu utatekelezwa vipi? wakati mwingine itabidi utekelezwe kwa lazima, na ukifanya hivyo wajinga watazidi kupata sababu ya kuwadanganya wenzao wasichanjwe sababu zina "matatizo"...
Kumbe na wewe ubongo wako ni mdogo kama wa mamba!?,kuona watu kwenye foleni ndo unadhani watu wamekubaliana na chanjo!?,fanya research ndogo, pita mtaa wowote katika mkoa wowote uliopo jaribu kuuliza watu tofauti tofauti kuhusu chanjo, majibu utayapata.

Fanya hivyo hata kwa wiki nzima. Walio tayari kuchanjwa huwezi kuwakosa, Ila waweza wasifike hata 1% ya watanzania milioni 60. Tusibezane mnaotaka mkachanjwe, wengine hatuchanji hata kwa mtutu wa bunduki.
 
Kumbe na wewe ubongo wako ni mdogo kama wa mamba!?,kuona watu kwenye foleni ndo unadhani watu wamekubaliana na chanjo!?,fanya research ndogo, pita mtaa wowote katika mkoa wowote uliopo jaribu kuuliza watu tofauti tofauti kuhusu chanjo, majibu utayapata. Fanya hivyo hata kwa wiki nzima. Walio tayari kuchanjwa huwezi kuwakosa, Ila waweza wasifike hata 1% ya watanzania milioni 60. Tusibezane mnaotaka mkachanjwe, wengine hatuchanji hata kwa mtutu wa bunduki.
Unadhani walioko kwenye foleni za chanjo wanaenda kupiga selfie halafu wanaondoka? wewe ndio uende huko vituoni ukajionee.
 
Binafsi sina tatizo na fikra au mawazo yako haya. Na in fact kuhusu "insubordination" hilo halina ubishi, ni kweli kutotii na kufuata "order" ya aliye juu yako ni kosa kubwa lenye adhabu kali...

Lakini hebu tujiulize, kuwa, Je ni kweli kila kitikacho kwa mkubwa huyu ambaye ni binadamu tu aliye sawa na wewe kwenda kwa subordinates wake ni kamili/sahihi/,ukweli na hakina kasoro au hatari yoyote...?

Itakuwa ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu kama mtu anakubali na kutii chochote toka kwa binadamu mwenzake na kisha kukitenda bila kwanza kukiweka au kuliweka jambo hilo vipimo vya kiusalama wa kwanza ROHO na kisha MWILI...!

Nimalizie comment yangu kwa kusema hivi;

Kwamba, hii ishu ya chanjo ya UVIKO 19 ni vita ya katika falme mbili wa MUNGU YEHOVA na wa SHETANI/IBILISI. Ni vita/mgogoro wa kiimani. Ni majira ya kubagua kondoo na mbuzi...

Ni ishu ya mtu binafsi kufanya uchaguzi awe au afuate upande upi kwa maslahi na usalama wake wa sasa na wa baadaye...

It's a big challenge. Lakini wenye misuli ya imani katika Kristo Yesu watashinda...!

Asante
 
Uzi mzuri ..

Pascal, I agree with you 100% especially serikali inavyopaswa kuwachukulia hatua watumishi wake wanaoiponda chanjo waziwazi..

Namna ulivyoondolewa TBC binafsi imeniuma but that's life..POLE kwa yote Brother.
Wanabodi,
Kwa vile zoezi la chanjo ya Uviko linaendelea, Kwa Maslahi ya Taifa inaendelea kujikita kwenye chanjo, leo nikiangazia hoja ya uhiari wa Chanjo. Japo chanjo ni hiari,...
 
Mi nashauri gwajima avuliwe uanacha kisha kamati kuu ikuteue uwe mgombea wa kawe.
The guy is a conman
Alisema keshanunua treni
Alisema anapeleka watu birmingham
Katukana serikali kwamba inaongozwa na wapinga kristu
Kakinzana wazi wazi na rais aliye madaraka ni kuhusu chanjo
Alimtukana hadharani cardinal pengo

sijaelewa serikali na ccm vinamucha huru

huyu jamaa ni proof kwamba even conmen are untouchable
 
Back
Top Bottom