Azam Sports Federation cup: Simba Vs Coastal Union | Benjamin Mkapa Stadium

Cross ya Kanoute imemkuta Baleke na kaipiga header lakini mpira umetoka nje na kuwa goal kick
 
Manzoki kaja kucheki game tu au Kuna mengine?
Hii ni update kutoka kwenye radio

Tueleze vizuri mkuu hiyo Manzoki amefata nini hapo kwenye kipindi ambacho dirisha dogo limefungwa?
 
Simba mpira hautembei. Nini zaidi?
Mi mwenyewe nashindwa kuelewa, hata Saido leo anaonekana hayuko vizuri

Sijajua nini shida japokuwa Coastal wamekuwa wasumbufu hata mechi ya mwisho tukiwa Tanga walitukazia sana kipindi cha kwanza tulitoka bila bila

Ngoja tuone second half naamini hii mechi tunashinda
 
Ukuta).jpeg

Simba imejenga ukuta wa Berlin
 
Uwanja umelowa ndiyo maana wachezaji wa Simba wanashindwa kucontrol mpira vizuri ingawa cha kushangaza Coastal Union hawaonekani kusumbuka sana kulingamisha na Simba.

Ila naona tumerudi kulekule kucheza mpira wa taratibu mno na kurudisha mipira nyuma. Mgunda amekaidi mfumo wa Robertinho.
 
Uwanja una maji?
 
Back
Top Bottom