Atakaye nisaidia kuipata simu hii natoa zawadi ya laki moja

Usiende TCRA mkuu ukienda ujue siri zako nyingine zote zinakuwa nje nje.
 
Hivi nikiokota simu na nikaamua kuitumia na mimi nakuwa ni mwizi?
 
Usiende TCRA mkuu ukienda ujue siri zako nyingine zote zinakuwa nje nje.
Wao ndio wanajua siri zako kuliko wewe hushangai uko peke yako chumbani una SMG yako unataka kumuuzia mtu umeiweka kwenye begi unatoka Mwanza unakuja Dar umeshaongea na mteja vizuri kwa njia ya simu unakuja kukamatiwa Ubungo
 
Mafundi wa simu wanachofanya ni kuUNLOCK hiyo IMEI no. baada ya wewe kuripoti na ikawa locked lakini hawawezi kubadili no. kwani zina maana yake. mfano zile 3 za kati kati ya hizo 15 ni Kampuni kuna toleo kuna aina na ni yangapi nk
ukiigia Google utakuta vyote IMEI

Nenda waulize mafundi wazuri hapo ulipo, wanabadilisha uzuri tu.
 
Nadhani huwa data ukiziweka kwenye simu ya android zinajiupload googledrive... Pia kuna option unaingia kwenye account yako ya googe then kwenye devices unauwezo wa kuactivate simu ikapiga makelele na aliyenayo akajulikana kuwa ni mwizi maana uwa inatoa saui kali kweli kweli.
Nirlekeze vizuri mkuu
 
Mm nimeibiwa simu ya kitochi
Ina data nyingi sana
Nikiziingiza kwa karatasi naweza jaza faili 5
Atakaeiona zawadi
250000
 
Wadau nimeibiwa simu yangu ya techno cx, ina nyaraka zangu za muhimu sana, kama kuna yoyote ataweza kunisaidia kuipata simu hiyo natoa zawadi tajwa hapo juu, imeibiwa maeneo ya magomeni dsm. Ni pm kwa taarifa zaidi.
Ndugu utaratibu wa taarifa kama hizo ni kwenda kutoa ripoti polisi na siyo mitandaoni labda kama unataka tujue tu kwamba umeibiwa simu
 
Wadau nimeibiwa simu yangu ya techno cx, ina nyaraka zangu za muhimu sana, kama kuna yoyote ataweza kunisaidia kuipata simu hiyo natoa zawadi tajwa hapo juu, imeibiwa maeneo ya magomeni dsm. Ni pm kwa taarifa zaidi.
Wahi polisi mkuu, wana kitengo.
 
Hao bora huo mda wa kwenda huko jamaa akahangaika kutafuta vitu vyake kwa njia nyengine,TCRA ukenda mara wanakwambia njoo na barua ya polisi kuthibitisha kama chombo ni chako police nao wanakamatia fursa utakaemkuta counter barua anataka akuuzie mara njoo na barua ya serikali za mitaa mara risiti za manunuzi.kibongo bongo ukishaibiwa simu kaa tulia fanya taratibu nyengine tu.
Mbona unakata tamaa hujui kama "zama zimebadilika" kuanzia kwenye tiba ya malaria mpaka utendaji wa kazi wa serikali
 
hapana IMEI inatokea kiwandani, na simu nyingi zina IMEI 2
hakuna fundi anayekubali kushika simu hizo kwani wengi wanakamatwa nazo za wizi au mtu aliyeuawa hivyo wamekoma.
simu nyingi smartphone ukInstall Google Map na uwe na acc ya Goole itaonesha mahali ilipo muda wote wa uhai wake ma kukuletea mawasiliano kwenye email yako
kuna app nyingi za kuinstall usiibiwe na kuendelea kutumika
POLISI wanasaidia hii kitu


Mkuu Ukwaju, naomba kufahamu hayo maujanja... Niinstall apps zipi ili simu ikiibiwa niweze kuikamata kwa urahisi.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom