#COVID19 Askofu Gwajima ni mpotoshaji sana suala la Chanjo za COVID-19

KITUGA

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
529
610
Sijawahi kuanzisha uzi hapa lakini baada ya kusikiliza clip ya Gwajima jana nilikereka sana na uongo wake.

Hakuna Shirika linaitwa emergency drug authorization USA kuna FDA Food and Drug Administration sio Flag and Drug Administration na ndio Regulatory Authority pekee ya vaccine drug and food na hao ndio waliotoa emergency use authorization ya Pfizer and Moderna vaccine.

Ukiangalia kwa makini utaona nchi nyingi duniani zimefanya utafiti na nyingine zinaendelea na utafiti lengo ni kuokoa maisha ya watu wao huyu Askofu alipinga chanjo kanisani kwake akiziita ni mpinga kristo jambo ambalo si la kweli kabisa.

Hivi huyu Gwajima na Mbowe nani ni akili kubwa? Mbowe ana uelewa mkubwa sana ndio maana alichanjwa na kukiri baada ya kusoma wafatiti wanasemaje na uasilia wa maendeleo ya program ya vaccination dunia nzima tafiti zinapingwa na tafiti sio uropokaji.

Anasema FDA haijauthorize chanjo wakati si kweli FDA ndio imetoa emergency authorization ya vaccination ya Pfizer na Moderna vaccines.

Ukiangalia mitandaoni watu wengi wanamsupport sababu elimu ya Corona vaccine TZ bado ni ndogo sana wataalam wana kazi kubwa ya kuwaeleza wananchi umuhimu wa corona vaccine sio kupotosha kama Gwajima.

Gwajima alisema kanisani kwake 5G technology inasambaza corona sio kweli kabisa nchi nyingi pamoja na TZ zina corona lakini hazina 5G technology.

Anasema corona vaccine imeharakishwa sawa ni kweli kutokana na maendeleo ya technology na hii golden age ya vaccinology ni kupongeza wataalam na tafiti za mRNA zilianza toka milipuko ya SARS na MERS viruses hatuwezi kuacha millions ya watu wanakufa kisa technology ya zamani ili chukuwa 8 years.

Utaalam wa corona awaachie virologists epidiomogists watafiti na madoctors yeye achunge kondoo wake na kuongea uongo uko sio bungeni.
 
Ukiangalia mitandaoni watu wengi wanamsupport sababu elimu ya Corona vaccine TZ bado ni ndogo sana wataalam wana kazi kubwa ya kuwaeleza wananchi umuhimu wa corona vaccine sio kupotosha kama Gwajima.
emoji1548.png
emoji1548.png
emoji1548.png
emoji1548.png
 
Hapo ndo ushangae kama mbunge wa kuchaguliwa na wananchi akili zake ziko hivyo, hao wananchi waliomchagua si ndo misukule kabisa

Mimi nasubiria safari ya kwenda Birmingham. Ahadi ni deni
Huyu ni wale wateule wa Mwendazake Dikt Magufuli kupitia maigizo ya uchafuzi mkuu. Lakini kwa bahati mbaya ndio wako bungeni (90%) kufanya maamuzi kwa niaba ya wananchi. Muumba ampumzishe anakostahiki!
 
Nilihisi anadanganya kama alivodanganya kuwapeleka watu Barmingum sijui

Anajaribu kummanipulate mama, lakini atakwama kama kweli hiyo kamati ipo.

Hayo mataifa yanayochanja si kwamba walipokea tu hizo chanjo na kuanza kuchanja raia wao. Walizifanyia uchunguzi si kama maneno matupu anayoyatoa gwajiboy.

Kwa taarifa yake: Hivi sasa raia ndio wanazihitaji hizi chanjo hakuna anaelazimishwa.
 
Mimi alivyosema tu FDA ya USA kirefu chake ni Frag and Drug Authority badala ya Food and Drug Administratin, NIKAACHA KUMSIKILIZA

Gwajima ni Mzungumzaji mzuri sana (Orator) anayetumia stori za vijiweni + utaalam wa kushawishi na kuzungumza ili kuwapoteza watu.
 
Tumpuuzeni Gwajima Ila hoja yake tuibebe!

Kama wengi wenu mlivyo mpuuza Hayati JPM Kwenye maamzi mengi kuhusu Corona, Ila hoja ya kutokuilock nchi tuliibeba wote ndivyo tunapaswa kufanya Kwa Askofu Gwajima

Gwajima, ameshauri Jambo la maana mno hatuwezi kuipuuza hoja yake kisa alimtoa jimboni kipenzi chenu
 
Inaonekana unaogopa sana kufa eeh?
Kwa imani yangu uhai ni zawadi ambayo Mungu amempa kiumbe wake.

Askofu Gwajima hakufanya utafiti wa kutosha kwanza FDA anasema ni Flag and Food Administration badala ya Food and Drug Administration pili mRNA anasema MRA kwa kujirudia.

Anasema kuna shirika linaitwa Emergency Drug Authorization ndilo lililoruhusu hizo vaccines za US huo ni uongo mkubwa tena, Regulatory Authority ya Vaccines Drugs na Food ni moja US ambayo FDA ndio ilifanya emergency use authorization ya Pfizer na Moderna vaccines sababu ya transmibility au maambukizi ya haraka sana na rate ya vifo vingi huyu Askofu anazidi kusema uongo mbele ya Bunge.

Awe kimya kama wabunge wenzake kwenye masuala ya Kitaalam Raisi ameunda time ya wataalam tuipe muda itakuja na report yake sio kuropoka uongo tu bungeni.

Halafu dunia nzima inahangahika na hili janga watz wengi walipotoshwa sana na madhara yake yako mpaka sasa kwani ukiaangalia mitandaoni ile isiyo makini wengi wanampongeza huyu mpotoshaji sababu ya kuwa brainwashed na wanasiasa.

Na hili liwe fundisho kwa nchi za Kiafrika Viongozi wa kisiasa wana ushawishi mkubwa sana kuliko wataalam wakiabuse hizo nguvu zao kuna madhara makubwa na ya muda mrefu.

Mungu anapenda nchi zote duniani sio Tanzania peke yake na tusiwe kisiwa hata nchi ndogo majirani zetu zinatushinda kwenye uelewa wa mambo nyeti ya sasa duniani.

Awamu ya 5 ilipatia kwenye kukataa lockdown lakini masuala mengi ya Corona kulikuwa na mismagement kubwa sana na kutokujipanga Mama ana kazi kubwa kutudisha kwenye mstari mmoja na Dunia.
 
Una uhakika hujawahi kuanzisha uzi humu au umesahau? Hujui kama JF ina rekodi zako zote?
 
Back
Top Bottom