Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 912
- 4,247
Kuna jumbe mbalimbali za maandishi zimeanza kusambaa kwenye page za wapinzani zikionyesha askari wa polisi wakilalamika kwamba baada ya kufanya kazi miaka 30+ wameambulia kikokotoo kisichozidi milioni ishirini.
Mmoja nimeona amesema anashindwa hata kurejea kijijini kutokana na kwamba fedha hizo haziwezi kufanya kitu chochote .Je ni kweli kwamba kuna mtumishi anastaafu analipwa kiinua mgongo milioni kumi na nane ambayo ni mshahara wa mwezi mmoja wa mbunge?
Wengine wanalalamika kwamba zaidi ya askari na maafisa 2000 wamegoma kustaafu na wamepewa mkataba wa miaka miwili. Najiuliza kama miaka 30 walishindwa kujipanga wataweza kujipanga ndani ya miaka hii miwili? Lakini. Kibaya zaidi ni kwamba hata viongozi wakubwa wa jeshi nao wamekataa kustaafu na kuongezewa miaka miwili ambapo ipo wazi kwamba kisiasa mikataba hii inapunguza presha za uchaguzi ila tunaamini hawa wanaopewa mkataba wataondoka na maumivu ya kikokotoo hiyo 2026?
Ila pia kwanini badaya yakuendelea kuwaretain kwanini hizo fedha zisiongezwe kwenye kikokotoo? Lakini pia hawa askari 2000 wanazuia vijana wangapi wasiajiriwe?
Mimi nadhani hadi askari wameanza kuandika meseji kwa akina X mayor Jacob na kundi lake maana yake wamefikia mahali wamekosa pakusemea. Niombe IGP na wenye mifuko ya jamii wakae na askari na kuwaandaa waweze kustaafu kwa amani.
Natambua kwamba wananchi wengi wanaoshabikia hizi jumbe kule mtandao wa tweeter wakidai kwamba askari wengi wamejitakia lakini sioni kama ni sahihi kuendelea kuwahukumu.
Jengeni tabia yakujadiliana ndani kama ambavyo majeshi mengi yalikuwa yanafanya miaka ya 1970 hadi 1990. Hao askari wadogo wengi hawana nyumba na wanasomesha bado. Tusiwapuuze wala kuwekeza kuwatafuta kupitia cyber ; tujiulize hadi wanaanza kuwaamini akina Jacob tumekosea wapi?
Lakini pia nimemsikiliza Mbowe Kagera, ametembea na agenda hizi hizi. Na anaungwa mkono na makundi mengi kwenye hii hoja hivyo ni vyema tukakubaliana kwamba waliofilisi mifuko siyo askari wala watumishi wa umma.
Mshahara wa mwezi mmoja wa mbunge uwe ndiyo pensheni ya askari wa miaka 60? Let us rethink.......tumekosa sana sana