Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,541
113,691
Haki Sio Hisani-Nipashe 06:06:21.png

Wanabodi,

Kila siku za Jumapili, huwa ninaandika makala za "Kwa Maslahi ya Taifa", makala ya wiki hii ni kuhusu hoja ya "Haki sio hisani, ni stahiki".

Japo hakuna binaadamu yoyote anayefurahi kifo cha mtu yoyote, kifo chochote kinapotokea, kinahesabika ni mpango wa Mungu, na kama kawaida watu hulia kumlilia marehemu, na baada ya kifo, hufuatiwa na mabadiliko ama hasi, ama chanya, tumeshuhudia familia nyingi zimefiwa na baba mwenye nyumba, na mama kuachiwa peke yake mzigo wote wa kulea familia, ikitarajiwa familia ingetetereka, lakini mambo yakawa tofauti, huyo mama mjane akapa power ya ajabu, akawa na uwezo wa kuilea familia yake vizuri na wakawa na ustawi kuliko hata alipokuwepo baba mwenye nyumba, hivyo msiba ule, kuonekana kama ulikuwa ni blessing in disguise. Hivyo ndivyo hali ilivyo kwa ujio wa rais Mama Samia, awamu iliyopita suala la haki za watuhumiwa wa uhalifu, lilikuwa ni kama hisani ya DPP, viongozi, jeshi la polisi na mahakama, lakini tangu rais Mama Samia ameapishwa, agenda ya haki ni moja ya vipaumbele vyake, hivyo kifo cha JPM kilichomleta rais Mama Samia, is like a "blessing in disguise", kufuatia kilio cha haki kwa watuhumiwa, kupata sikio la kukisikia, na sasa Watanzania, wanakwenda kutendewa haki na amini usiamini, huu mchaka mchaka wa haki Samia alioanza nao, anaweza kuendelea nao hadi kutupatia katiba mpya!.

Hii ni sehemu ya pili ya mfululizo wa makala za "Kilio cha Haki ", kuwaonyesha jinsi DPP aliyepita alivyofifisha haki, ili kumsaidia DPP mpya, kuisafisha ofisi ya DPP, ili mambo kama yale, yasijirudie, ila pia haki nyingine, zilikuwepo kwenye katiba, zikanyofolewa, sasa tunaomba zirudishwe.

Nakumbushia nilipoishia wiki iliyopita
Ni kwa muda mrefu Nchini kumekuwa na kilio cha haki kutoka kwa watu na asasi za kiraia, watu wanapigwa risasi mchana kweupe kwenye maeneo yenye ulinzi, na hakuna uchunguzi wowote!, watu wanapotea na wengine wanaokotwa kwenye viroba, hakuna uchunguzi wowote, Watu wanaswekwa mahabusu na kuozea jela kwa miaka na miaka bila kesi zao kusikilizwa, Kilio hiki cha haki, kimekuwa kikiangukia kwa viziwi kutoka kwa mamlaka, lakini kuja kwa Samia Suluhu Hassan kama rais mpya wa Tanzania, ingawa alikuja tu kwa bahati mbaya kufuatia kifo cha rais JPM, na Watanzania kumlilia sana Magufuli wetu, ujio wa rais Samia, sio tuu amekuja kuwafuta Watanzania machozi, ujio wake ni kama Baraka fulani, Samia ana jicho fulani kali, linajua kuponye na kuona mbali, limeona kilio cha haki kwa Watanzania, na kujitolea sio tuu kuwafuta Watanzania machozi, bali kuliponya taifa. Mtu muhimu kabisa wa kuyateleleza haya ni DPP.

Watuhumiwa Wakirushwa Kichurachura.jpeg
Huu ni udhalilishaji watuhumiwa!, lengo la kuwachuchumalisha watuhumiwa na kuwarusha kichurachura ni ili kuwa contain wasitoroke, hebu tuambiane ukweli, kweli Mzee kama James Rugemalira, kwa umri ule, na Seth kwa umbo lile, kweli hawa ni watu wa kuchuchumalishwa na kurushwa kichurachura ili kuwadhibiti wasitoroke?. Halafu askari magereza wanajisikia very proud kuwafanyia mahabusu vitendo hivi, huku wakiwasubiri waandishi kuja kuwapiga picha!.

Kanuni za Msingi za Haki
Tanzania inafuata Mfumo wa Sheria wa Kiingereza, ambao unafuata misingi ya haki ambayo ni pamoja binadamu wote ni sawa na wana haki sawa mbele ya sharia, kila mtu anahesabika hana hatia mpaka athibitishwe na mahakama, jukumu la kuthibisha hatia ni la upande wa mashtaka, hakuna mtu anayehukumiwa bila ya kusikilizwa, hakuna mtu anayehukumiwa mara mbili kwa kosa lile, na hata ukikutwa na hatia, unayo haki ya kukata rufaa. Kwenye haki za kisiasa, haki kuu ni haki ya kila Mtanzania kugombea nafasi yoyote ya uongozi, toka serikali ya mtaa hadi serikali, lakini haki hii ilikuja kuporwa kwa kulazimisha kugombea nafasi yoyote ni lazima udhaminiwe na chama cha siasa, huku ni kuwalazimisha Watanzania kujiunga na vyama kwa lazima. Turejeshe haki hizi kwenye katiba yetu.

Vyombo vya Utoaji Haki, Visipo Tenda Haki, Mungu Huingilia Kati na Kutoa Adhabu ya Karma
Sijajakutana na mtuhumiwa yeyote, kabla ya kuandika makala hii, kwa sababu hakuna atakayekubali, lakini kile kilichompata James Rugemarila, Harbinder Singth Sethi na Joseph Makandege, au wale Mashehe wa Uamsho, kinajulikana kwa kila mtu nchini Tanzania, kulingana na vyombo vya habari. Hawa na watu na wengine wengi wanasota na kuteseka katika magereza ya Tanzania kwa kukosa haki, kwa miaka na miaka, kesi zingine huu ni mwaka wa nne watu wako mahabusu, hata usikilizwaji wa kesi zao bado haujaanza, ma Shehe wa uamsho, huu ni mwaka wa 8!. Watu hawa na wengine wengi, japo ni watuhumiwa tuu, lakini hata watuhumiwa wanastahili haki. Kwa waumini wa kitu kinachoitwa karma kama mimi, naamini karma ya kilio cha haki, kwa watu kulia kwa kumwaga machozi, jasho na damu, kwa ukosefu wa haki kunakofanyika Tanzania, kwa Watanzania wenzetu, inaweza kuwa inawaponza na kusabisha kuondoka mapema kwa baadhi ya wapendwa wetu, ambao sisi tunawapenda na lakini Mungu anaamua kuingilia kati kwa kuwapenda zaidi na kuwaita kwake!.

Kesi ya James Rugemarila, Harbinder Singh Sethi na kesi ya Mashehe wa Uamsho ni Mfano Hai
James Rugemarila, Harbinder Singh Sethi na Joseph Makandege wameshtakiwa kwa makosa ya uhujumu wa uchumi na utakatishaji fedha, Dola za Marekani 151,569377.52 na TZS 8,522,219,917.44. Pesa hizi ziliwekwa chini ya akaunti ya escrow huko BOT, walishinda kesi hiyo, mahakama iliamuru serikali walipwe, pesa zilitolewa na kulipwa kwao kwa amri ya mahakama, kupitia miamala ya benki, na rekodi zote za kila muamala zipo, hii ndio inayoshangaza na wengi wetu, ni uchunguzi wa aina gani ambao unachukua muda mwingi hivi wakati fedha zilikuwa BOT hapa hapa, zikachotwa na kuhamishiwa benk nyingine mbili n azote zipo hapa hapa nchini?, sasa huu ni mwaka wa 4 uchunguzi bado unaendelea, ni uchunguzi wa aina gani huu?

Uko wapi Usawa Kabla ya Sheria?
Kifungu cha 7 cha Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu (UDHR) kinasema: "Watu wote ni sawa mbele ya sheria". Kila mtu lazima atendewe sawa sawa chini ya sheria bila kujali rangi, jinsia, kabila, dini, ulemavu, au sifa zingine, bila upendeleo, ubaguzi au upendeleo. Tamko hilo limeingizwa kwenye katiba yetu, hivyo ukiukwaji wowote wa haki za binaadamu ni ukiukwaji wa katiba!.

Kwanini Serikali Haikukata Rufaa Kupinga Uamuzi wa Mahakama? Usawa Mbele ya Sheria Uko Wapi?
Ikiwa serikali haikuridhika na uamuzi wa mahakama IPTL walipwe, kwanini hawakukata rufaa?!. Haya na tukubali kuwa IPTL waliiba fedha hizo, ikiwa ni kweli waliiba fedha hizo, pesa hazikujibadilisha mikono yzenyewe zikatoka BOT kwenda kwenye akaunti za IPTL, walihamishiwa kisheria, ikiwa uhamisho huo ni wizi , kwanini ni James Rugemarila tu, Harbinder Singth Sethi na Joseph Makandege pekee?, watu wa BOT walitoa fedha hizo wako wapi? wapi Majaji walioamuru IPTL wako wapi maafisa wa serikali walioidhinisha malipo hayo?. Usawa uko wapi mbele ya sheria?

Hakuna Mtu Anayehukumiwa Bila Kusikilizwa, Kwanini Uhukumu Watu Jela Bila Kuwasikiliza?
Wakati kesi hii bado inasubiri kusikilizwa huku uchunguzi bado ukiendelea, ni zaidi ya miaka minne sasa, watuhumiwa wote wako gerezani, kwenye kesi ya Uamsho, Mashehe wale wako gerezani kama mahabusu kwa mwaka wa 8 sasa!. Kuna tofauti gani kwa mtuhumiwa anayekaa miaka 4 au 8 gerezani kama mahabusu, kusubiri kesi yake kusikilizwa, na mfungwa aliyehukumiwa kifungo cha miaka 4 au 8 jela?. Kitendo cha mahabusu, kukaa miaka 4 hadi 8 mahabusi ni kama wamehukumiwa bila kusikilizwa. Vifungo vya miaka 4 na miaka jela!. Kanuni ya haki inasema, "Hakuna mtu anayehukumiwa bila kusikilizwa", Iko wapi dhana ya kutokuwa na hatia mpaka uthibitishwe?, Na hata ikitokea kesi hiyo ikasikilizwa na watuhumiwa hao wasipokutwa na hatia, hakuna kiwango cha fidia unaweza kuwalipa kuwafidia muda wao wote uliowashikilia gereza bila hatia.

Hakuna Mtu Atakaye Shitakiwa Mara Mbili kwa Kosa Hilo Hilo ”, Angalia Hapa Nini Hiki Kinafanywa na DPP Wetu?
Kana kwamba yote hayo hayatoshi, serikali yetu ilikiuka kanuni nyingine ya haki ya asili ambayo inasema "hakuna mtu anayehukumiwa mara mbili kwa kosa moja". Huku DPP, akifungua kesi ya jinai ya uhujumu na utakatishaji fedha ya Dola 151,569377.52 na TZS 8,522,219,917.44 . DPP huyo huyo akafungua Kesi nyingine ya mada, Kesi Na. 90 ya 2018 kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati dhidi ya IPTL, kampuni inayomilikiwa na James Rugemarila na Harbinder Singth Sethi ambapo serikali inadai madai ya Dola 151,569377.52 na TZS 8,522,219,917.44 . Yaani serikali uwashitaki watu kwa jinai ya wizi wa fedha na hapo hapo kufungua kesi ya madai kuzidai fedha hizo hizo!. Yaani fedha hizo huku ni jinai na fedha hizo hizo ni fedha halali.

Je, Serikali Yetu Pia Inasafisha Pesa Chafu? Je, Huu Sio Usafishaji wa Pesa?
Unapowashitaki watu kwa kosa la jinai la uhujumu wa uchumi na utakatishaji fedha, hiyo inamaanisha fedha hiyo inayotakatishwa ni fedha chafu, fedha ya wizi, ni ama zimeibwa, ama zimepatikana kwa njia isiyo halali, lakini serikali hiyo hiyo iliyofungua kesi ya jinai, ya utakatishaji fedha, halafu wakati huo huo, kufungua kesi nyingine ya madai ukidai pesa ile ile, kwanza ni kinyume cha sharia ya double jeopardy lakini hii inamaanisha nini kwa serikali inayodai hii ni pesa chafu iliyoibiwa, katika kesi moja ya jinai, halafu ifungue kesi nyingine, ya madai na kutafuta suluhu ya amani?. Kitendo cha kuigeuza pesa iliyopatikana kwa jinai ya uhalifu, na kuja kudai fedha hizo hizo kwenye kesi ya madai, huu sio utakatishaji wa fedha kwa njia za kiserikali? . Je kuna tofauti gani kati ya hatua hii na zile za serikali zinazosafirisha mihadarati ili kupata pesa za kuendesha serikali yao?

Kama Kanuni ya Haki ni Mtu Asishitakiwe Mara Mbili kwa Kosa Lile Lile, Hiki Kinachofanywa na DPP, ni Nini?
Kwa maoni yangu, sio haki kwa DPP kuwafungulia watuhumiwa kesi ya jinai ya uhujumu wa uchumi na Utakatishaji fedha, halafu hapo hapo, wakafungua kesi nyingine ya madai, kwa DPP huyo huyo kuzidai tena fedha hizo. Watuhumiwa wamekaa gerezani kwa zaidi ya miaka 4 sasa tangu wakamatwe. Kwa hivyo, Serikali haikuwa na ushahidi wa kutosha kuwashtaki watuhumiwa lakini kesi ya madai ambayo sasa imesuluhishwa Mahakamani, ingekuwa ya kutosha kutoa madai yake.

Ninaandika maoni haya wakati ninajua hali ya kesi za uhujumu na utakatishaji wa fedha, upelelezi haujakamilika hadi leo huku watuhumiwa wamekaa gerezani kwa zaidi ya miaka 4 sasa bila kesi, kusikilizwa, hiyo ni kinyume na Kifungu cha 29 (6) cha Sheria ya Uhujumu [Sura 200 R.E. 2019] kile kinachotoa; "Ambapo Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma au ofisa mwingine wa umma, baada ya kusoma jalada la kesi ya polisi na taarifa za mashahidi waliokusudiwa, ana maoni kwamba ushahidi uliopo hautoshi kuidhinisha kushtakiwa, ilimbidi asipeleke kesi mahakamani. Wenzetu Afrika Kusini, upelele unafanywa hadi ukamilike ndipo washitakiwa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani na kesi yao kusikilizwa, upepelezi gani huu wa miaka zaidi ya minne?.
Hhhh
Tukutane wiki ijayo kumalizia kilio cha haki, Sehemu ya Tatu na ya mwisho kwa kutoa mapendekezo kwa DPP.

Paskali
 
Pasco Mayalla sasa ni Kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM.

Operation HAKI by CDM! asante samia for that anyway!

Pascal Mayalla No one is concerned with you being a Kada of CCM, everybody's concern is YOU and YOU to side with KILLERS, ABDUCTORS, MALICIOUS PROSECUTORS, ELECTION RIGGERS, HUMAN RIGHTS VIOLATORS and the like.
 
Hatuko tayari kuona wazalendo wa nchi yetu wakinyanyaswa na wauza madawa ya kulevya.

Tunaanza kampeni rasmi ya kumchangia na kumuwekea wakili Sabaya kwenye kesi yake. Kama msaliti wa nchi mzee wa MIGA aliweza kuchangiwa ,sisi kama watanzania wazalendo hatuwezi kushindwa kumchangia Sabaya ambaye kwa uzalendo wake aliitoa wilaya ya Hai kutoka ya 63 kwenye ulipaji kodi hadi ikawa ya 4 kitaifa...
Hili sio ajabu, ni kawaida kwa CCM kutetea majambazi maana CCM na ujambazi ni kitu kimoja.

Pambaneni ninyi kwa ninyi, wapinzani tumekaa pembeni tunawaangalia tu vile mnatifuana.

Lissu aliwahi kusema mkitumaliza sisi mtaanzana ninyi kwa ninyi
 
Hili neno "haki" enzi ya mwendazake lilikuwa gumu sana kutamkwa, afadhali sasa hivi linatamkwa, ila hiyo haki unayoitaka ya kubadilisha katiba itakusababishia usipewe cheo chochote huko CCM, sometimes unajipendekeza vizuri, sometime unaharibu hata hueleweki.
 
Mkuu, credibility yako humu JF machoni mwa members wengi imeshuka sana kutokana na kujitangaza kuwa wewe ni kada wa hii CCM dhalimu ya sasa. OK, mtu anaweza ku argue kuwa kada wa CCM linaweza lisiwe tatizo - but kunyamazia au kuunga mkono ushetani unaofanywa na CCM hii ya sasa ni jambo jingine kabisa ndugu.

Mimi ni CCM lakini siyo hii CCM iliyokengeuka na kuwa dhalimu kiasi hiki. Mimi ni CCM ile ya Mwalimu (RIP baba yetu).
 
Hatuko tayari kuona wazalendo wa nchi yetu wakinyanyaswa na wauza madawa ya kulevya...
Usitumie neno Uzalendo ili kuhallalisha uovu.

Anayetaka kumchangia jbazi Sababya, na afanye hivyo. Lakini watu wa haki na wana wa Mungu, kama walivyomlilia Mungu, naye akajibu kwa mkono wenye nguvu, wataendelea kuomba ili wale wote waliodhulumu na mawakala wao wakutane na mkono wa Mungu.
 
View attachment 1812108

Wanabodi,

Kila siku za Jumapili, huwa ninaandika makala za "Kwa Maslahi ya Taifa", makala ya ya wiki hii ni kuhusu hoja ya "Haki sio hisani, ni stahiki"...
Paschal naona baada ya dikteta kutwaliwa umeanza kurudi kwenye ubora wako, Paschal wewe ni mwandishi mzuri sn sema njaa na tamaa vilikupitia hapa katikati. Nashukuru umeanza kujirekebisha, sisi tuna taka haki hata uwe CCM au upinzani haki lazima itendeke
 
Mkuu, credibility yako humu JF machoni mwa members wengi imeshuka sana kutokana na kujitangaza kuwa wewe ni kada wa hii CCM dhalimu ya sasa. OK, mtu anaweza ku argue kuwa kada wa CCM linaweza lisiwe tatizo - but kunyamazia au kuunga mkono ushetani unaofanywa na CCM hii ya sasa ni jambo jingine kabisa ndugu...
Naona ameanza kurudi kwenye ubora wake, Paschal andaa muda ujibu maswali yetu hapa kwanini ulikengeuka kipindi cha dikteta na utuombe radhi sisi ni binadamu tutakusamehe.
 
Hatuko tayari kuona wazalendo wa nchi yetu wakinyanyaswa na wauza madawa ya kulevya.

Tunaanza kampeni rasmi ya kumchangia na kumuwekea wakili Sabaya kwenye kesi yake. Kama msaliti wa nchi mzee wa MIGA aliweza kuchangiwa, sisi kama Watanzania wazalendo hatuwezi kushindwa kumchangia Sabaya ambaye kwa uzalendo wake aliitoa wilaya ya Hai kutoka ya 63 kwenye ulipaji kodi hadi ikawa ya 4 kitaifa...
Tutabadilisha katiba kipengele cha Term limits tuziondoe Mama atawale milele. Mbona wapuuzi nyie mtakoma.
 
Paschal naona baada ya dikteta kutwaliwa umeanza kurudi kwenye ubora wako, Paschal wewe ni mwandishi mzuri sn sema njaa na tamaa vilikupitia hapa katikati. Nashukuru umeanza kujirekebisha, sisi tuna taka haki hata uwe CCM au upinzani haki lazima itendeke
Hapana, huyu ni mnafiki, akija mtu kama Jiwe, tarudi huko huko kutafuta kuteuliwa! achana naye huyu ni nyoka ndumila kuwili. Njaa inamhangaisha asijue la kufanya au aegamie wapi maana mama hamjui Pascal Mayalla hivyo si rahisi kumpa uteuzi (I know, huwa analetewa wa kuteua, sidhani kama wote anawafahamu personally.
 
Back
Top Bottom