Aliyepandisha gharama za Toto Afya kadi ni muuaji. Magufuli tunamkubuka kwa hili

The Burning Spear

JF-Expert Member
Dec 23, 2011
3,445
8,305
Kama unatibiwa india. Au unatoka familia yenye ukwasi huwezi kujua mateso wanayopata watanzania wa kawaida..

Watu wanatumia mitishamba au kwenda kwa mwaposa badala ya kwenda hospital kukwepa gharama kubwa za matibabu. Uongo mkubwa wanakwambia mtoto chini ya miaka 5 anatibiwa bure.

Hata kwa watu wazima vifurudhi vya bima siyo rafiki sana na huduma ni mbovu. Ni mateso makubwa taifa linaangamia.

Hukohuko NHIF wanakosema mfuko umezidiwa fedha zinagawanwa kama njugu nchi ngumu sana hii..

Screenshot_20230922-223413.jpg
 
Wakati mwingine , ni ile ya malipo ni hapa hapa.
Ni Hawa Hawa wanaoumia na gharama za matibabu au huduma mbaya.
Ndio hao hao watetezi wa udhalimu,rushwa na matumizi mabaya ya watawala.

Acha waendelee kuimba mama anaupiga mwingi.
 
Waziri Ummy Mwalimu aliporudishwa wizara ya afya ndio kaja kutuharibia sababu watoto wake wanatibiwa nje ya Nchi. Hana moyo wa Uzalendo, mda wote anakenua kenua kinafki
Na bado.
Bado matokeo ya bandari kuuzwa ndiyo utaita maji mma
 
Wanadai watoto waliokuwa Wana tibiwa kwa kifurushi Cha Toto Afya walikuwa wachache,aise! Hii nchi kila mtu anajiamulia anavyotaka hasa akiwa na mamlaka bila kufikiria watu wengine wataathirika vipi.

Eti wamehamishia kwa watoto wanaosoma waunganishwe kwa magroup,swali linakuja kwa watoto ambao hawajfikia umri wa kwenda shule wanapataje hizo huduma za bima ya afya?

Wananchi hawana chao maana maswala Kama haya ilitakiwa kuwashirikisha wananchi njia gani itakuwa Bora zaidi kupatiwa huduma ya afya kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya afya.

Watanzania wengi tuna hali ngumu lakini serikali inazidi kutukamua kila siku inasikitisha Sana.
 
Nyie ndio mnawapigia kura, Hawa akina mama wanatakiwa wakalee familia na wajukuu uongozi wamefeli hawawezi. Watazidi kuharibu Nchi kwa ulimbukeni na udhaifu walio nao
Nipange foleni nikampigie mtu ambaye hana uchungu na nchi?
Hata km sina kazi, ni bora nikachukue jembe nikalime.
 
Wanadai watoto waliokuwa Wana tibiwa kwa kifurushi Cha Toto Afya walikuwa wachache,aise! Hii nchi kila mtu anajiamulia anavyotaka hasa akiwa na mamlaka bila kufikiria watu wengine wataathirika vipi.

Eti wamehamishia kwa watoto wanaosoma waunganishwe kwa magroup,swali linakuja kwa watoto ambao hawajfikia umri wa kwenda shule wanapataje hizo huduma za bima ya afya?

Wananchi hawana chao maana maswala Kama haya ilitakiwa kuwashirikisha wananchi njia gani itakuwa Bora zaidi kupatiwa huduma ya afya kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya afya.

Watanzania wengi tuna hali ngumu lakini serikali inazidi kutukamua kila siku inasikitisha Sana.
Hii nchi ni ngumu sana.
 
Kama huwezi lea, usizae

Sasa kwa akili ya kawaida 50400 ndo itumike kugharamikia matibabu?

Wangejiunga watu 1mil hakika isingefutwa
Libya waliwezaje kutoa matibabu bure kwa wananchi wake?

Halafu huduma za serikali wanadai wananchi wanachangia tu sio kwamba ndio malipo stahiki kwa huduma husika mfano huduma za afya.

Kwa rasilimali Zote hapa Nchini inashindikana vipi serikali kuwahudumia wananchi wake kwa gharama nafuu?

Akili za viongozi sio bunifu kabisa....kwenye Mambo muhimu Kama afya serikali ingetengeza mfumo wa kukusanya maokoto kwa ajili ya huduma hizi na sio kumkandamiza mwananchi wa kawaida.
 
Shida ya toto bima ilikuwa wengi wa waliojiunga walikuwa ni watoto wenye changamoto za Kiafya
ili mfuko wa bima uwe na uwezo ni lazima kuwe na wachangiaji ambao hawatatumia fedha za mfuko kwa mwaka husika.
 
Libya waliwezaje kutoa matibabu bure kwa wananchi wake?

Halafu huduma za serikali wanadai wananchi wanachangia tu sio kwamba ndio malipo stahiki kwa huduma husika mfano huduma za afya.

Kwa rasilimali Zote hapa Nchini inashindikana vipi serikali kuwahudumia wananchi wake kwa gharama nafuu?

Akili za viongozi sio bunifu kabisa....kwenye Mambo muhimu Kama afya serikali ingetengeza mfumo wa kukusanya maokoto kwa ajili ya huduma hizi na sio kumkandamiza mwananchi wa kawaida.
Nenda Libya kaishi
 
Nchi ya Majinzi na selfish hii, Wacha tuendelee kuwashtaki kwa Mungu, yatakuwa na mwisho mbaya, wizi wao hautawafaidisha chochote.
 
Waziri Ummy Mwalimu aliporudishwa wizara ya afya ndio kaja kutuharibia sasa ivi watoto wetu wanateseka kupata matibabu. sababu watoto wake wanatibiwa nje ya Nchi. Hana moyo wa Uzalendo, mda wote anakenua kenua kinafki
Ukiendelea kuongelea pumba za uzalendo utakufa hivu hivi unajiona.

Tafuta hela Mzee. Hakunaga uzalendo, ni mwendo wa kibepari tu, huja hela unakufa!
 
Wanadai watoto waliokuwa Wana tibiwa kwa kifurushi Cha Toto Afya walikuwa wachache,aise! Hii nchi kila mtu anajiamulia anavyotaka hasa akiwa na mamlaka bila kufikiria watu wengine wataathirika vipi.

Eti wamehamishia kwa watoto wanaosoma waunganishwe kwa magroup,swali linakuja kwa watoto ambao hawajfikia umri wa kwenda shule wanapataje hizo huduma za bima ya afya?

Wananchi hawana chao maana maswala Kama haya ilitakiwa kuwashirikisha wananchi njia gani itakuwa Bora zaidi kupatiwa huduma ya afya kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya afya.

Watanzania wengi tuna hali ngumu lakini serikali inazidi kutukamua kila siku inasikitisha Sana.
Hili la ambao hawajifika umri wa kwenda shule ndio jambo
 
Back
Top Bottom