Aliyeng’atwa ulimi kushtakiwa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,565
21,562
Majeruhi wa kung’atwa ulimi, Saidi Mnyambi (26), amefunguliwa shtaka la kujaribu kubaka.

Mnyambi ambaye aling’atwa ulimi hadi kukatika na mwanamke kwenye tukio la ngono, ‘kibao’ kimemgeukia na yuko chini ya ulinzi wa polisi wodi namba nne alikolazwa kwa takriban wiki moja akituhumiwa kwa jaribio la ubakaji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Peter Kakamba amesema wanamshikilia Mnyambi baada ya awali kumkamata Mwajabu Jumanne (36) kwa tuhuma za kujeruhi kwa kung’ata ulimi.

“Tumelazimika kuwashikilia wote wawili kutokana na kila mmoja kumtuhumu mwenzake. Baada ya uchunguzi wa kina tutafikia maamuzi stahiki,” amesema.


Chanzo: Mwananchi
 
36-26! Huyo dogo inaelekea anapenda sana 'mimama'!:):)
 
Hata mi nilihisi kua jamaa alitaka mzigo kwa nguvu kwa sababu jirani kalewa ndio akang'atwa ulimi

Ngoja tuone serikali itaamua nini ?
 
Back
Top Bottom