Ajali za mabasi ni janga la kitaifa, serikali yapeni umuhimu stahiki maisha ya wasafiri

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
38,269
47,485
Hizi ajali za barabarani za mfululizo za mabasi zinazomaliza maisha ya watu na kuwafanya maelfu kuwa walemavu ni kama zimekuwa jambo la kawaida sasa na kuzoelekana.

Inasikitisha sana kuona Waafrika hatuyapi maisha thamini na hadhi inayostahili. Ajali mfululizo za mabasi za aina hii zinazotokea nchini kwetu zingekuwa zinatokea katika ulimwengu wa magharibi huenda zingeiondoa hata serikali madarakani kwa kura za raia au za bunge za kutokuwa na imani na serikali. Hili Bunge letu kwa nini halitimizi wajibu wake wa kuisimamia serikali katika mambo muhimu kama haya?! Ajali tatu za mabasi zinazoua makumi ya raia kwa mwaka zilitosha kuunda kamati maalumu lakini mpaka sasa bunge letu ni kama halina habari kuhusu jambo hili!

Serikali kwa sababu hamna jawabu sahihi kuhusu hizi ajali fanyeni haya kwa kuanzia wakati tunasubiri reli.

1. Ondoeni haya mabasi makubwa ya abiria 40, 50 hadi 60 kwa safari za masafa marefu. Safari za umbali unaozidi kilometa 200 zitumuike gari zinazobeba abiria wasiozidi 30 tu ili kama hata kuna ajali wafe wachache.

2. Magari ya mizigo ya masafa marefu yatembee saa kumi mbili asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni tu.

3. Gari lolote litakaloharibika barabara kubwa(highways) lisikae barabarani zaidi ya lisaa moja. Polisi, afisa wa LATRA, Mwenyekiti wa kijiji au mtaa anapopata taarifa kuna gari limekaa barabarani zaidi ya lisaa limoja awe na mamlaka ya kuliondoa na kulitupa pembeni mbali na barabara kokote kule kwa njia yoyote ile.

4. Basi zote za abiria mwisho wa kusafiri kwa siku moja iwe ni masaa 12 tu , kama safari ni zaidi masaa 12 au KM 800 abiria wakate tiketi zaidi ya moja za mabasi tofauti.

5. Dereva mmoja wa basi za abiria endeshe gari kwa masaa 6 tu au KM 400 kwa siku.
 
#4 naunga mkono
 
Bunge la tanzania lipo kuitetea serikali na kusapoti maamuzi ya serikali hata kama ni ya hovyo ,kwaio usilitegemee kwa jema. Hayo mapendekezo yako sioni tija yake, Kikubwa wananchi tunatakiwa tujitambue na serikali iliyopo madarakani ikae pembeni kupisha akili mpya maana imexpire katika kusimamia nchi.
 
Hizi ajali za barabarani za mfululizo za mabasi zinazomaliza maisha ya watu na kuwafanya maelfu kuwa walemavu ni kama zimekuwa jambo la kawaida sasa na kuzoelekana.

Inasikitisha sana kuona Waafrika hatuyapi maisha thamini na hadhi inayostahili. Ajali mfululizo za mabasi za aina hii zinazotokea nchini kwetu zingekuwa zinatokea katika ulimwengu wa magharibi huenda zingeiondoa hata serikali madarakani kwa kura za raia au za bunge za kutokuwa na imani na serikali. Hili Bunge letu kwa nini halitimizi wajibu wake wa kuisimamia serikali katika mambo muhimu kama haya?! Ajali tatu za mabasi zinazoua makumi ya raia kwa mwaka zilitosha kuunda kamati maalumu lakini mpaka sasa bunge letu ni kama halina habari kuhusu jambo hili!

Serikali kwa sababu hamna jawabu sahihi kuhusu hizi ajali fanyeni haya kwa kuanzia wakati tunasubiri reli.

1. Ondoeni haya mabasi makubwa ya abiria 40, 50 hadi 60 kwa safari za masafa marefu. Safari za umbali unaozidi kilometa 200 zitumuike gari zinazobeba abiria wasiozidi 30 tu ili kama hata kuna ajali wafe wachache.

2. Magari ya mizigo ya masafa marefu yatembee saa kumi mbili asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni tu.

3. Gari lolote litakaloharibika barabara kubwa(highways) lisikae barabarani zaidi ya lisaa moja. Polisi, afisa wa LATRA, Mwenyekiti wa kijiji au mtaa anapopata taarifa kuna gari limekaa barabarani zaidi ya lisaa limoja awe na mamlaka ya kuliondoa na kulitupa pembeni mbali na barabara kokote kule kwa njia yoyote ile.

4. Basi zote za abiria mwisho wa kusafiri kwa siku moja iwe ni masaa 12 tu , kama safari ni zaidi masaa 12 au KM 800 abiria wakate tiketi zaidi ya moja za mabasi tofauti.

5. Dereva mmoja wa basi za abiria endeshe gari kwa masaa 6 tu au KM 400 kwa siku.
Nyuzi kama hizi hazina wachangiaji wengi subiria sasa, za aslay na Simba na yanga.

Kulishutumu bunge sio sana maana bunge mda mwingine linaenda na trend, kama kuna kitu kinaongelewa sana kwenye social media na kina umuhimu lazima bunge lijadili tu.

Hivyo kama kungekuwa na malalamiko ya wananchi lazima wangejibu tu lakini sisi watu wenyewe tuna puuzia.

Utakuta dereva yupo mwendo kasi lakini watu hawachukui hatua, mda mwingine gari linatoka stand brake hamna lakini watu wanaona poa tu "eti Mungu yupo" nadhani ilitokea Ile ajali ya basi toka tandahimba liliua zaidi ya 20
 
Mleta mada ametoroka Milembe? Kwamba yatumike mabasi ya abiria 30 kupeleka abiria Dar-Bukoba au Dar Musoma? Mahesabu ya kiuchumi yamekaaje?

Mfumo ni mzuri wa usimamizi wa mabasi kupitia LATRA, ni kuongeza usimamizi wa taasisi zaidi ya mmoja ili mfumo uwe na internal auditing. Kuna watu wanacheza na watu wa LATRA magari yao hayaonekani kuzidi spidi. Kama mfumo unaangakiwa na zaidi ya mtu mmoja, hofu itakuwepo.

Hujatupatia hata takwimu za ajali per idadi ya mabasi
 
Miundombinu pia ifanyiwe kazi kupunguza maeneo hatarishi.

Vitu kama michepuko vilimani, barabara zipanuliwe kwenye kona hatarishi maana bado hatuna uwezo wa kujenga "dual carriageway" kwa umbali mrefu.

Magari yakaguliwe na kuhakikisha yana ubora na vigezo stahiki kuingia barabarani. (Kuna ajali zinasababishwa na gari kukosa taa au viashiria kwa nyuma wakati wa usiku, na kupelekea gari lingine kugonga kwa nyuma)

Tuwe na magari ya kuondoa gari zenye matatizo (breakdown) barabarani, gari lisikae zaidi ya lisaa katikati ya barabara.

Gari bovu likiwa barabarani kama ishara za usalama hazijawekwa inavyopaswa, kuwe na fine kubwa (na kuwe na road patrol kwa ajili hiyo).

Askari wa usalama barabarani na wadau wengine wawe na weledi na sio kuweka kipaumbele kukusanya pesa za kipigia viatu brashi.
 
Yaani hizo basi za watu 50/60 kutokana na ukubwa na nafasi iliyopo mzinga wake hawafi watu wengi, ingekuwa coaster hapo ya watu 30 asingetoka mtu hata mmoja.
Mengine naunga mkono
 
Mleta mada ametoroka Milembe? Kwamba yatumike mabasi ya abiria 30 kupeleka abiria Dar-Bukoba au Dar Musoma? Mahesabu ya kiuchumi yamekaaje?

Mfumo ni mzuri wa usimamizi wa mabasi kupitia LATRA, ni kuongeza usimamizi wa taasisi zaidi ya mmoja ili mfumo uwe na internal auditing. Kuna watu wanacheza na watu wa LATRA magari yao hayaonekani kuzidi spidi. Kama mfumo unaangakiwa na zaidi ya mtu mmoja, hofu itakuwepo.

Hujatupatia hata takwimu za ajali per idadi ya mabasi
Itakuwa hujasoma au hujaelewa point namba 4 pamoja na hilo gharama za mafuta na posho kutoka Dar es Salaam hadi Bukoba havizidi Milioni 1, kwa bus la abiria 30 wanaolipa 100,000 bus linaingiza Milioni 3.
 
We jamaa bhana,Mchawi hapo ni kuboresha barabara tu na kuzipanua.Barabara zetu mabasi yanapita hilo,mbuzi,bajaji,Bodaboda,waendao kwa miguu,mbwa,yani kila aina ya gasia
 
Yaani hizo basi za watu 50/60 kutokana na ukubwa na nafasi iliyopo mzinga wake hawafi watu wengi, ingekuwa coaster hapo ya watu 30 asingetoka mtu hata mmoja.
Mengine naunga mkono
Kuna bus za abiria 30 au hata 20 ambazo sio coaster.
 
Hiyo namba 1 hapana. Gari dogo safari ndefu ndo linaua vizuri pakitokea ajali halafu gharama ya usafiri itakuwa kubwa.

Barabara zetu nazo nyembamba mno. Yaani tuna barabara nyembamba hakuna pa kutorokea kunapohitajika kukwepa kwa dharura. Halafu pamoja na wembamba zina mawimbi makubwa makubwa sasa na mabasi haya yakiwa speed saa yoyote linaweza mshinda dereva.

Nilipanda basi la Marangu usiku yaani kuna eneo basi unahisi lipo speed 120 ila muhudumu anasema basi linaenda 50 top 70 hazidishi hapo ila hali ya barabara hata hiyo 70 unaona ni kasi mno, unatamani aende hata 40 mchelewe. Gari inayumba, barabara nyembamba.
 
95% ya ajali zinazotokana na mabasi zinasababishwa na uzembe wa madereva wenyewe kama wewe ni mfatiliaji mzuri wa mambo ya barabarani utaelewa hili
 
Nilipanda basi la Marangu usiku yaani kuna eneo basi unahisi lipo speed 120 ila muhudumu anasema basi linaenda 50 top 70 hazidishi hapo ila hali ya barabara hata hiyo 70 unaona ni kasi mno, unatamani aende hata 40 mchelewe. Gari inayumba, barabara nyembamba.
Huna sababu ya kuhisi pakua app ya kupima mwendokasi wa chombo ulichopanda uwe unafatilia wewe mwenyewe
 
Back
Top Bottom