TANZIA Agnes Gerald ‘Masogange’ afariki dunia Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge, Dar

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,520
2,092
Wadau nilipita Mama Ngoma Health Centre Mwenge na kukuta watu wakilia kuuliza naambiwa Video Queen Masogange amefariki muda mfupi uliopita.

Masogange.jpg

=========
UPDATES:
=========

Video queen maarufu Bongo Agness Gerald maarufu kama Agness Masogange amefariki Dunia leo katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyoko Mwenge, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Alikuwa anasumbuliwa na Homa ya matumbo pamoja na tatizo la kupungukiwa na damu.

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.

Habari zaidi....

Mwanamitindo na video queen marufu bongo Agnes Gerald maarufu kama Masogange, amefariki dunia jioni ya leo April 20 alipokuwa amelazwa katika hospital ya Mama Ngoma akipatiwa matibabu

Akithibitisha taarifa ya kifo hicho Daktari Rama Ngoma wa hospitali ya Mama Ngoma, amesema Agnes amefariki dunia kwa tatizo la pneumonia na upungufu wa damu jioni hii, na alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta.
Tayari mwili wake umeshatolewa hospitali ya Mama Ngoma, na kwa mujibu wa muigizaji Steve Nyerere umepelekwa hospitali ya Taifa ya muhimbili.

Agnes Masogange alikuwa maarufu baada ya kuonekana kwenye video kadhaa za bongo ikiwemo Masogange ya Belle 9.

Je ugonjwa wa pnemuonia (Nimonia) ni nini?

Pneumonia ni maambukizi katika viriba ya hewa katika pafu moja au mapafu yote. Viriba hivi vya hewa huweza kujaa maji au usaha na kusababisha mgonjwa kukohoa, homa kali na kupumua kwa shida. Pneumonia hubebwa na bakteria, virusi au fangasi.

Habari zaidi, soma=>Ufahamu undani wa ugonjwa wa pneumonia (Nimonia)
 
Wana JF Msaniii Agness Masogange ameaga dunia Leo jijini Dar Es Salaam. Taarifa zaidi hivi punde.
Wameona wamtangulize maana angetaja mabosi wake wanaomtumiaga kwenye kusafirisha ngada. Ni kama yule aliyesema Lowasa ni baba yake, alipotaja tu na kuomba msamaha mabosi wamemgeuka, sasa anacheza segere la Polisi peke yake.

All in all, RIP.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom