Afisa Habari Simba: Wachezaji Wanadai Bonus zao Na Club haina Pesa

Smart codetz

Senior Member
Jan 25, 2023
190
753
Meneja Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally Amekiri wachezaji wa Timu hiyo kudai bonasi.
" kweli wachezaji wanadai Bonasi zao za mechi kadhaa, Kuna wakati taasisi inakuwa na fedha inalipa madeni yote Kuna wakati haina fedha inalimbikiza madeni Mzigo ukipatikana watu wanalipwa"

Ahmed Ally Ameongeza kuwa ni kawaida kwenye taasisi ya biashara watu kucheleweshewa miezi miwili au mitatu lakini hiyo sio sababu ya kufungwa na Azam FC " wametufunga mara mbili wametuzidi ubora "



News & Video Credit: @SokaPlace
63F9687F-330D-4003-90B4-F465063F777A.jpeg
 
Meneja Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally Amekiri wachezaji wa Timu hiyo kudai bonasi.

" kweli wachezaji wanadai Bonasi zao za mechi kadhaa, Kuna wakati taasisi inakuwa na fedha inalipa madeni yote Kuna wakati haina fedha inalimbikiza madeni Mzigo ukipatikana watu wanalipwa"

Hivi hawa si ndio wale walikataa udhamini ili waweke nembo ya " Visit Tanzania"...?

Sasa watani mmeona jinsi siasa zinavyo wavua nguo? Haya timu haina pesa ya kulipa wachezajli Bonasi, mtatoa wapi pesa za kuwavunjia mikataba wachezaji hewa ambao wengi wao wamebakiza mwaka mmoja mmoja kwenye mikataba yao?

Pia mtapata wapi pesa za kusajili mmbadala wa wakina Onyango, Putin na Baleke?

Upi umuhimu sasa wa kuwapo kwa Mo Dewji (Rais wa. heshima) klabuni kwenu?

Mnakosaje tupesa tudogo tudogo twa kuwalipa wachezaji bonas zao.

Mechi ya Yanga mliwaahidi kuwalipa wachezaji mil 350 kama tu wakiwafunga Yanga SC. Mpaka sasa hivi Boss Mo ndo kagoma kaabisa kupokea simu.

Try Again na genge lake wako bize kwenye ofisi za Mbet wakiomba mkopo wa kumaliza maadeni ya Bonasi kwa Wachezaji. Wakati huo huo Mo anawaangalia tu, Ni tajiri gani huyo?

Anyway sioni wa humzuia Yanga SC kutwaa ubingwa msimu ujao wa 2023/24.
Screenshot_20230509-141631898.jpg
 
Back
Top Bottom