Afande Sele amchana Sugu, adai hajafanya lolote bungeni kutetea muziki, Sugu ajibu

Mbilimbi Mbovu

Senior Member
May 25, 2015
185
119
page2.jpg
​

Rapper Afande Sele amesema wasanii hawajanufaika na ubunge wa Joseph Mbilinyi aka Sugu licha ya kumsaidia kumpigia kampeni katika uchaguzi uliopita.

A
kizungumza na Planet Bongo ya East Afrika Radio, Afande alisema Sugu ameshindwa kuwatumikia wasanii na kujinufaisha yeye mwenyewe.

Sisi tuliamini akienda kule ndio mdomo wetu, kasahau kabisa wasanii wenzake, alisema. Kipindi ambacho wasanii wa antivirus wanalalamika kwamba kawatosa porini, akasema yeye sio mbunge wa wasanii ni mbunge wa Mbeya. Huyu ni msaliti kwa wenzake, sasa mtu msaliti namna hii jinsi kumuondoa ni sisi kuamua kuingia bungeni wenyewe kupigania maslahi yetu, aliongeza.

Baada ya kauli hiyo, Sugu amemjibu kwa kusema kuwa yeye hakuwa mbunge wa wasanii bali alikuwa mbunge kwaajili ya watu wake wa Mbeya mjini.

Nafikiri hafuatilii bunge, unajua uzuri wa vitu vya bunge vinaenda kwa rekodi, labda atakuwa hafuatili bunge. Lakini kwa wanaofuatilia bunge wanajua. Mimi sio mbunge wa wasanii, mimi ni mbunge wa Mbeya mjini, alisema Sugu.

Kwahiyo chochote ninachokifanya bungeni ninakifanya kwa mapenzi yangu na pia kama waziri kivuli. Kwa msanii anayefanya kazi sawa ila kwa mtu anayelala lala kama yeye lazima atakufa njaa. Lazima utakufa njaa lakini kwa msanii kama Professor Jay, msanii kama Shetta wana- appreciate kazi ambayo tunaifanya bungeni kwa kauli zao.


Chanzo: Bongo5
 
Sasa ulitaka atumikie wanamziki au mziki au wananchi wa jimbo lake?maana katika wananchi na wanamziki wamo humomo.wewe bwana wewe
 
Afande sele anahaha huku na huko kutafuta KICK, hatimaye kaipata kwa kupewa ukweli!
 
Kero za wananchi wa Mbeya sio muziki ni barabara,maji,na vitabu madawati tu.sasa muziki wa nini? Itakuwa ni kuwakilisha usichotumwa.
 
Sugu hakuchaguliwa na wasanii,alichaguliwa na watu wa Mbeya mjini na anawatumikia wana Mbeya mjini...
Wakati Sugu anahangaika kuupata ubunge hao wasanii walikuwa kwenye majukwaa ya maccm wakiwanadi wagombea wa ccm,walimsaidia nini?leo wanataka awe mbungevwa wasanii
 
Afande sele ni bendera tu, upepo wako ni ZZK na Unajishusha hadhi kwa upeo wako mfupi sana wa kuona yanayotendwa na Sugu katika masuala ya maendeleo jimboni mwake.

ACT mnachokifanya ni kushambulia wapinzani ili kuzigawa kura zao na kuwapa CCM ushindi.

ZZK akihamia chama kingine na wewe utakuwa nyuma kama kawaida...... na je, huyo ZZK wako kawatetea vipi wasanii?
 
Huyo Afande Sele hajielewi, anasahau kuwa Joseph Mbilinyi ni mbunge wa wananchi na siyo wasanii.. Au ndo anavyolelewa ACT..
 
Bange zilishamuharibu tangu alipokimbia jeshi

Huyu hajitambui, badala ya kujituma ili a pate mafanikio analaumu watu bila sababu. Hajiulizi kwani hao wanamuziki waliofanikiwa wamesaidiwa na nani? Eti anakaa na kujidanganya aingie bungeni. Atasubiri sana. Yeye akale ndumu tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom