Recent content by Baba Vladmir

  1. Baba Vladmir

    Gesi tumboni

    Nilishaandika hapa mara nyingi juu ya tatizo hili na namna ya kujiponya.Fuatilia hizo nyuzi utapata msaada vizuri.
  2. Baba Vladmir

    Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

    Hapo anatakiwa atafute tiba tu hakuna namna.Huwezi kuugua malaria ukajitibu kwa kulala kwenye neti,hutapona.Bamia zinasaidia kutokupata tatizo na sasa tatizo ameshalipata,kwa hiyo lazima ajitibu apone halafu ndiyo aendelee na huo utaratibu,vinginevyo atamaliza magunia bila kupona.
  3. Baba Vladmir

    Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

    Ndiyo.Unaposema presha maana yake chanzo kikuu huwa ni kwenye moyo.Moyo wenyewe pamoja na mishipa yake mikuu inayotoa ama kuingiza damu kwenye moyo pamoja na mishipa mingine midogomidogo inayosambaza damu sehemu mbalimbali za mwili.Vyote hivi vinatakiwa kuwa kwenye utimamu wake,vinginevyo kasoro...
  4. Baba Vladmir

    Punguza unywaji wa pombe, ukiweza acha kabisa

    Madhara ya pombe ni makubwa sana kuliko wengi wanavyofikri.Mimi niko kwenye tiba kwa miaka kadhaa sasa,magonjwa mengi yanayowasumbua watu ni yale ya mtindo wao wa maisha ikiwemo unywaji wa pombe kupindukia. Wewe unayedharau na kupuuza ujumbe huu ambao umekufikia bure kabisa bila malipo ni wazi...
  5. Baba Vladmir

    Punguza unywaji wa pombe, ukiweza acha kabisa

    TAMBUA UNYWAJI SAHIHI WA POMBE Kitu cha msingi kwenye pombe siyo kujua aina ya beer au kilevi. Kitu cha msingi ni kujua percentage of pure alcohol (asilimia ya pombe halisi) na ujazo wake ( volume). Unit moja ya pombe ni sawa na 10mls of pure alcohol or 8g of the same. Mwanaume hutakiwa kunywa...
  6. Baba Vladmir

    Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

    Nenda kapime vipimo vya moyo.
  7. Baba Vladmir

    Afrika ndiyo kinara wa kufanya kazi ngumu lakini kisukari ni tishio je kazi ngumu sio mbadala wa mazoezi?

    Na hii ndiyo sababu kubwa hasa ya vijana wengi kuwa na kisukari. Asilimia ndogo sana ambayo inapata kisukari cha kurithi, lakini asilimia kubwa ni ulaji wa hivyo vitu ulivyovianisha. Kuna uhusiano mkubwa sana wa mlundikano wa mafuta mwilini na kisukari aina ya pili(type 2 diabate).
  8. Baba Vladmir

    Afrika ndiyo kinara wa kufanya kazi ngumu lakini kisukari ni tishio je kazi ngumu sio mbadala wa mazoezi?

    Ulaji wa vyakula vya mafuta kupindukia,jambo linalosababisha mafuta mengi mwilini na unene kupindukia. Mambo haya huambatana na ugonjwa wa sukari ambao zamani uliwaandama watu wenye umri angalau miaka 50. Lakini siku hizi mtu anakuwa na unene uliozidi akiwa na miaka michache.
  9. Baba Vladmir

    Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

    Unaweza kwenda kitengo cha mifupa pale mhimbili.Au kama utahitaji tiba mbadala unaweza kunijulisha pia tukaona namna ya kushauriana na kusaidiana.
  10. Baba Vladmir

    Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

    Kwa historia ya muda ulioanza kupata shida hiyo,kuna uwezekano mkubwa ukawa na ugonjwa wa mifupa(Osteoporosis) ambao umeshindwa kuutibu muda mrefu na sasa umeendelea kujijenga na hatimaye unaonyesha kuwa limekuwa tatizo kubwa.Ugonjwa huu una sifa ya kupungua kwa molekuli ya mfupa na kuzorota kwa...
  11. Baba Vladmir

    Matumizi mabaya ya dawa zilizohalalishwa

    Namna ambavyo watu hutumia madawa kujitibu ni kama vile kutumia nyundo kubwa kuua buibui.Siku hizi watu wengi wananunua madawa kutoka katika maduka ya dawa bila kuwaendea wataalamu wa afya waliobobea.Wakati mwingine madawa ya kawaida kwenye maduka ya dawa yanaweza yasiwe mazuri na hata kuwa na...
  12. Baba Vladmir

    Baridi yabisi (Arthritis): Ugonjwa wenye tiba maelfu

    UGONJWA WA BARIDI YABISI NI NINI? Baridi yabisi ni neno la jumla kwa magonjwa au michakato mingine isiyo ya kawaida itokeayo kwenye viungo. Mamilioni ya watu ulimwenguni kote wanaugua aina fulani ya baridi yabisi. Viungo vyetu na mishipa yetu, kama ilivyo misuli yetu, hudhoofika kadiri...
  13. Baba Vladmir

    Bawasiri imenikata nguvu za kiume kabisa, msaada aliyepona

    Dawa zipo tena za uhakika,isipokuwa wagonjwa wengi wanapenda kutapeliwa.Mfumo wa tiba una kanuni zake,haijalishi ni mitishamba.Mtu ana tatizo la miaka mitano lakini anataka atumie dawa siku mbili apone kweli!
  14. Baba Vladmir

    Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

    Pole.Una umri gani sasa na tatizo umeanza kuliona lini?
Back
Top Bottom