Viatu vya culture

Mar 26, 2020
47
54
Waheshimiwa habari zenu,

Naomba kuuliza na kufahamu, viatu vya culture kwa hapa DSM wanatengeneza wapi au wanapouzia kwa jumla? Msaaada wakuu nina tanguliza shukrani

Naweka picha ili upate kujua nachoulizia

4ae9e4dd-2bb6-4352-8a57-803bae8d3560.jpeg
bae4ea3e-d90d-4040-a94f-196c5abc67c7.jpeg
76de2fa6-e889-450c-86c5-08009b96c637.jpeg
 
Nenda Machinga Complex pale jengo la kwanza kama unaelekea kariakoo achana na lile la pili kama unaelekea boma au buguruni.

Pale Machinga Complex chini kabisa wala hupandishi kwenda juu/ngazi. Utakuta watu wa kutengeneza viatu, shanga na mambo mengineyo. Hapo ndo naona viatu vingi vya kimasai vinatengenezwa.

Ila quality ya kiatu itategemea na gharama. Wengi pale wanatengeneza viatu vya bei ya chini 5000, 7000, 8000 (bei za reja reja). Hapo wengine wanajumua na kuja kuuza mtaani 10,000, 12,000 unaweza uziwa hadi elfu 15 ukajuwa ni original.

Ila ukitaka kiatu original hapo inabidi uonane na fundi mwenyewe ukae naye chini myajenge.
Maana kiatu cha kimasai chenyewe original makamilisho yake kila kitu huwa inafika elfu 10,000 au zaidi kutegemeana na uwa au style ya kiatu chako, vile vile material yanayotumika (Ngozi, soli, sponji, karpet na nk).

Kwa uzoefu wangu rakini. Fanya uchunguzi wako pia ukifika pale au kwa mafundi wa viatu mtaani watakupa maelezo maana kalibia mafundi wengi wana chukulia baadhi ya vifaa hapo Machinga.
 
Asante sana boss wangu
Ulikua sahihi kwa asilimia 95%
Shukran
 
Back
Top Bottom