SoC02 Tabia zetu hutufanya tuwe tulivyo kiuchumi

Stories of Change - 2022 Competition

Alley67

New Member
Jul 20, 2021
1
0
Saikolojia inasema ukifanya kitu kila siku kwa siku 21 kitu hicho hugeuka na kuwa tabia, hivi Ulishawahi kujiuliza kwanin nafanya kitu au biashara kama anavyofanya mwingine lakini sifanikiwi, au mbona mimi lakini sio fulani kiufupi binadamu tumeumbwa kujifananisha na kujilinganisha na wengine na baada ya kujithibitishia kuwa tumezidiwa kwa namna moja au nyingine kama vile kiuchumi au kimaisha kwa ujumla maranyingi hujaribu kuiga ili tufanane nao mfano kuna mtu huwa ukimuona kavaa nguo dizaini fulani na kupendeza akili hukutuma kununua nguo ya dizaini hiyo huku ikiamini pia na wewe utapendeza bila kujali aina ya mwili wako

TABIA
  • Humfanya mtu kuamini yupo sawa na kuwa mgumu kubadilika
  • Humumfany mtu kufanya kitu kile kile hatakama hakipendi
  • Humfanya mtu kutambulika katika jamii kutokana na tabia yake mfano kitu kikiibwa utasikia hapa lazima fulani ndiye kaiba
  • Humpa mtu nafasi fulani kama anakubalika mfano kazi ikitokea hata kama hujaomba unaweza kupewa
Tabia ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila siku na hukupa uwezo wa kukufanya uwe jinsi ulivyo mfano tuchukulie watu wawili wenye uwezo wa kupokea mshahara wa million 5 kwa mwezi, mmoja akawa na tabia ya kupanga budget kabla msharaha haujatoka na kuufanyia kama budget ilivyopangwa na mwingine akawa na tabia ya kuusubiri mshahara na baada ya kuupokea ndiyo matumizi yanaanza. Watu hawa hatakama wana matumizi sawa ya kawaida lazima kuna tofauti itakuwepo katika maisha mfano kwa anaepokea mshahara ndio atumie ni vigumu sana kubaki na akiba kwani mara nyingi hujikuta hela ishakwisha bila kujua na hata kurudia na kupitia ni wapi alipotumia hela ni vigumu wengi hubaki kusema tu “pesa mwanaharamu”, “sijui hata imeishaje” na anaweza kuhisi ameibiwa na mtu wake wa karibu

Aidha tabia za kutopenda mafanikio ya wengine pia huturudisha nyuma na kutufanya sisi pia tusifanikiwe mfano Mtu hapendi ndugu yake kabisa wa damu afanikiwe kwa sababu tu yeye anataka awe na mafanikio zaidi yake, hii itamfanya asifanikiwe kwa kuw pengine ndugu yake angefanikiwa pia yeye kupitia kwake angeweza kufanikiwa na hata kumzidi lakini kwakua amemzibia milango ya kutokea na yeye pia anajizibia pasipo kujua kwa sababu tu anahisi hawez kumsaidia ndiyomaan waswahili husema “ TENDA WEMA NENDA ZAKO”

TABIA AMBAZO HUKUDUMAZA SIKU HADI SIKU
  • Kuchelewa kuamka : tabia hii hukufanya usiwe makini kwa siku nzima yaani asubuhi ikipita ukiwa haujatulia kifikra ni vigumu kufanya kazi zako kwa ufasaha
  • Kupenda kufanya kazi rahisi kwanza : kuna watu ambao wakifika kazini hupenda kuanza kufanya kazi rahisi au nyepesi kwanza kabla ya kufanya kazi nzito hii hupelekea muda wa kufanya kazi nzito kuwa wamechoka na hivyo kupungusa usabifu
  • Kuwa bize na simu kazini : sikuhizi simu imegeuka na kuwa sumu kwani kuna watu ambao huweza kupitisha siku bila kula lakini wawe tu katika mitandao hivyo huwezi kufanya kazi kwa umakini ukiwa na bize na simu yako.
  • Kutokuwa na malengo madogo na makubwa kwa siku,wiki, au zaidi : malengo ni muhimu sana katika maisha bila malengo mtu huweza kufanya kazi bila mafanikio na kuona hajakosea lakini hafanikiwi kumbe siri ni ndogo tu MALENGO, Jaribu Kuweka malengo ya siku wiki na zaidi
  • Kutokuwa tayari kubadilika au kuwa mgumu kushaurika: sio kila ushauri ni wa kufuata na sio vibaya kutumia akili yako lakini kuna watu pia huwa na ushauri ambao unaweza kubadilisha maisha yako kabisa, jaribu kuchuja na kuona baina ya washauri na ushauri wao naamini hutokosa kupata kitu
  • Kukubali kwa kila kitu kwenye kikao :
  • Kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja: maranyingi watu wanaofanya vitu vingi kwa wakati mmoja hushindwa kujikita zaidi hivyo kufanya kitu visivyo na ubora mfano unakuta mhandisi anafanya miradi zaidi ya minne kwa wakati mmoja na anataka yote iishe kwa muda hii itamfanya kuimaliza bila ubora ambao ungepatikana endapo angekuwa na mradi mmoja
  • Kuwa na chuki hasa kwa mafanikio ya watu wengine: Tukumbuke mafanikio ya watu wengine hayawezi kuzuia mafanikio yetu na badala yake yanaweza kuongeza mafanikio yetu kwa kujifunza kutoka kwao na pia kwa mtu aliyefanikiwa anaweza kukusaidia hata mtaji au wazo na ushauri lakini chuki na kuziba riziki humfanya mtu kushindwa kupiga hatua kwani hutumia muda na mawazo kutafuta jinsi ya kumdhoofisha mwenzake badala ya kujistawisha pia humfanya mtu kuwa huru bila kinyongo
  • Kutokupenda kutoa misaada kwa wenye uhitaji : Misaada humfanya mtu kuingiliana na jamii inayomzunguka kwani watu hukuachia baraka ambazo huwezi kuzipata popote pale na kwa gharama yoyote ile
  • Kuwa na kitu unachopoteza muda mwingi kisicho na faida: maranyingi watu huwa na vitu vinavyowafurahisha pale wanapochoka au pale wanapohitaji kupumzika mfano kusikiliza mziki, kuangalia filamu, kucheza michezo, kusoma vitabu, kubarizi ufukweni na vitu vingine vingi. Tabia hii sio mbaya kwani hukupa muda wa kumpisha akili ambayo huwa imechoka lakini tabia hii inapofanyika zaidi yaani kwa kupitiliza kipimo hugeuka na kuwa sumu ambayo hukupunguzia muda wa kuzalisha na kukufanya kuwa tegemezi kwake huku ukipoteza muda mfano mtu anayeperuzi mtandaoni kuangalia udaku kwa zaidi ya masaa 3 kwa siku humfany kupoteza masaa 21 kwa wiki ambayo ni sawa na siku nzima hivyo kwa kila wiki mtu huyu huperuzi siku moja nzima na kupumzika katika masaa matatu tu kwa siku hiyo

KINYUME cha tabia hizo ndio tabia zitakazokufanya ukue siku hadi siku kiuchumi na hata kifikra pia
 
Back
Top Bottom