chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 19,732
- 22,856
Nimemsikia Waziri wa Nishati Bw. Biteko akisema Serikali imelazimika kuzima mitambo ya kuzalisha umeme kwenye bwawa la Mwl Nyerere kwa kuwa matumizi ya umeme nchini ni madogo kuliko uzalishaji.
Nataka nimwambie Waziri Biteko kauli yake ya kuwa matumizi ni madogo SIYO KWELI bali ni kwamba UNIT moja ya umeme kwa bei anayouziwa mwananchi ni kubwa hivyo inalazimu watu kujizuia kutumia umeme kwa wingi, watu wanaogopa hata kutumia majiko ya umeme au heater ya kuchemshia maji kisa bei ya unit ipo juu. Shusheni bei ya umeme watu waachane na kuni watumie umeme kupikia.
Namshauri Waziri na bodi ya TANESCO wakae tena chini kufanya tena Mapitio ya gharama ya Unit za umeme.
Hatuwezi kusema tuna umeme wa kutosha mpaka kufikia kuzima mitambo huku bei ya umeme ipo juu. Vinginevyo tunakuwa tunadanyanyana.
PIA SOMA
- Biteko: TANESCO inanunua umeme wa Megawati 31 kutoka Uganda na Zambia
- TANESCO: Umeme tunaozalisha ni mwingi mahitaji ni madogo nchi nzima, hakuna mgawo kwa sasa