Mume kumsaidia mke kazi nyumbani siku ambayo haendi kazini ni wajibu au hiari?

SteveJr99

Senior Member
May 13, 2019
118
243
Tunajua wanaume ni viongozi na vichwa katika familia zetu na majukumu ya mwanamume na mwanamke huwa yanafahamika vizuri tu ndani ya nyumba.

Sasa ni kwanini siku ambayo mwanamume akipumzika nyumbani yaani haendi kazini mwanamke analazimisha kwamba umsaidie kazi na usipofanya ananuna hii ikanifanya niulize swali hili

Je, mwanaume kumsaidia mwanamke kazi nyumbani ni wajibu au hiari?
 
Tunajua wanaume ni viongozi na vichwa katika familia zetu na majukumu ya mwanamke na mwanamke huwa yanafahamika vizuri tu ndani ya nyumba.

Sasa ni kwanini siku ambayo mwanamume akipumzika nyumbani yaani haendi kazini mwanamke analazimisha kwamba umsaidie kazi na usipofanya ananuna hii ikanifanya niulize swali hili je mwanaume kumsaidia mwanamke kazi nyumbani ni wajibu au hiari?
Iwe kwa hiari na kwa maamuzi ya mwanaume mwenyewe. Hii habari ya kuona ni lazima nitoe msaada huo haipo..!!
 
Tunajua wanaume ni viongozi na vichwa katika familia zetu na majukumu ya mwanamume na mwanamke huwa yanafahamika vizuri tu ndani ya nyumba.

Sasa ni kwanini siku ambayo mwanamume akipumzika nyumbani yaani haendi kazini mwanamke analazimisha kwamba umsaidie kazi na usipofanya ananuna hii ikanifanya niulize swali hili je mwanaume kumsaidia mwanamke kazi nyumbani ni wajibu au hiari?
Fanya kazi za kiume Tu ,mfano kunavitu ambavyo vimearibika sio mpaka umwite fundi we mwenyew tu unaeza fix,
 
Ni wajibu wako kufanya hivyo na sio hiari,65%ya familia za sasa ni single mothers na ndio wanalea watoto pekee yao,wanaume wengi ni sperms donors
 
Tunajua wanaume ni viongozi na vichwa katika familia zetu na majukumu ya mwanamume na mwanamke huwa yanafahamika vizuri tu ndani ya nyumba.

Sasa ni kwanini siku ambayo mwanamume akipumzika nyumbani yaani haendi kazini mwanamke analazimisha kwamba umsaidie kazi na usipofanya ananuna hii ikanifanya niulize swali hili je mwanaume kumsaidia mwanamke kazi nyumbani ni wajibu au hiari?
Hao vilaza wa aina hiyo huwa mnawatoa wapi na hadi mnawaoa?
 
Tunajua wanaume ni viongozi na vichwa katika familia zetu na majukumu ya mwanamume na mwanamke huwa yanafahamika vizuri tu ndani ya nyumba.

Sasa ni kwanini siku ambayo mwanamume akipumzika nyumbani yaani haendi kazini mwanamke analazimisha kwamba umsaidie kazi na usipofanya ananuna hii ikanifanya niulize swali hili

Je, mwanaume kumsaidia mwanamke kazi nyumbani ni wajibu au hiari?
Kama wewe ndio unafanyiwa hivyo, ebu usitu jumuishe kwenye mambo ya kijinga kabisa...☹️
Na ole wako unijibu, nitakutandika khelbu sasa hivi...😕
 
Kwangu ni hiari na nina tafsiri kama upendo, sio masuala ya kulazimishana.

Kibaya sana mie mvivu mnoo na hivi vikazi vya nyumbani. So nikijisikia nafanya.
 
Kuoa sio kuwa mlemavu kwamba Kila kitu ni kuagiza tu.....lete kile, peleka hiki, toa pale, weka hapo wakati huo umekaa tu tangu asubuhi huna kazi yyt zaidi ya kuikumbatia rimoti. Tufanye kazi

Uvivu haufai
 
Mkuu nakushauri kama ww ni mwanaume usiskize ushauri wa kina dada hapo juu kuwa eti kufanya bila kuombwa huimarisha mapenzi,ngoja nikupe kisa changu Ndoa ya kwanza.
Nlisoma andiko gazeti flani la udaku kuwa kusaidia kazi za nyumbani Kwa mume kunaongeza mahaba,basi baba Ako nikawa nadamka asubaa naosha vyombo,nadeki naoga Kisha naenda kazini na wikiend ndio namsaidia hadi kupika.
Wiki za mwanzo nikawa naona manzi anatabasamu nikasema yes mambo yanajipa ila after another two weeks manzi akawa anachukia mara anatoa kasoro kwenye Kila nachofanya Nikaona huyu ashaniona houseboy,nikasema lazima nimlipue.
Kesho yake nimedamka nikafanya kama ninavyofanya na yeye kawahi akawa anakagua kama kawaida yake utadhani nyapara.Hasira zikanipanda nikamwachia vyombo nikavaa Kwa hasira nikaenda job.
Badae narudi anasema kabla hatujalala anamaongezi na mm dah nikasema hii kauli ya kisenge sipendi kuiskia niambie Sasa hivi au usiniambie kabisa,hapo Bado nahasira za asbuhi.
Basi akaanza pale oooh unadhani mm nitafanya nn kama ww unafanya kazi zote home?...dah nikamwambia mama kumbe ndio Hilo?Basi limeisha.Mpaka tunaachana na yule manzi sikuwahi osha hata kijiko.
N.B
Nakumbuka maneno yake ya mwisho wakati tunaachana alinambia eti mm Sina utu.
 
Ni Surprise, Huwa haitolewi kila siku au kwa mazoea na haina ratiba tena inatakiwa kua mara chache chache sana kwa kushtuliza ili kuithaminisha.
 
Tusaidiane endapo wote tunafanya kazi
Wote tunarudi tumechoka
Nikiwa naandaa dinner wewe unanisaidia kunyoosha nguo n.k
Sio lazima ila ni upendo tu wote tunachoka
 
Ukijaribu kufanya huo ujinga mwisho wa siku inakuwa mazoea, mwanaume kazi yako kutafuta hela! Sasa umeoa ili iweje kama bado unahangaika na kazi za nyumbani?
 
Back
Top Bottom