Swali kwako mke unayefanyakazi na kipato chako hakionekani!!

Mpiga Paspoti

JF-Expert Member
Dec 29, 2022
242
1,071
Idumu JF,

Namuuliza yule mwanamke ambaye kakubali kuolewa lakini anafanya kazi na kipato anachopata kazini anasema chake si cha familia!

Mume ni sawa anaitunza familia kwa huduma zote zinazompasa, na upendo kwa mkewe upo wa kutosha!!

Ninavyoelewa mimi ndoa ni muunganiko baina ya watu wawili (me na ke) mwende mkakabiliane na changamoto zenu; mtazokutana nazo hukoo ndoani thus why mke ambaye ni mama wa nyumbani anasimamia malezi ya watoto, usalama wa makazi, bajeti za nyumbani katika kuhakikisha mahitaji yanapatikana, kazi zote za nyumbani na kuhakikisha baba anakwenda kazini akiwa na furaha na amani!

Hayo ni majukumu mazito sana ambayo yumkini hata mama yako aliyabeba!!

Sasa wewe nyumbani huonekani ukiondoka asubuhi saa moja kurudi saa moja usiku, weekend Jumamosi kazini na Jumapili saloon!!

Wewe kama mama na mke wa familia, jukumu lako ni lipi hapo maana kipato chako hatukioni na nyumbani hupatikani! Malezi ya watoto na majukumu yote ya nyumbani yapo kwa dada wa kazi!! Umuhimu wako upo wapi?? Why niwe na uchungu nawe na nafasi yako siioni kama mke na mama watoto wangu??

Limenifika hapa! Hebu nifungueni pengine nitaelewa nikabadili mawazo!!
 
😅😅😅 Vumilia tu Mkuu- maana hapo bado hajakucheat na kukusengenya kwa watu kwa mabaya-Vumilia tu Mkuu- kwa maana huyo ndiyo chaguo lako
 
Umeoa corporate woman. Hao washazoea kua single mothers. Na huko makazini wanalishana sumu kali na mashosti!

Umeyakanyaga bro. Na mkiachana atataka kila kilichopatikana kupitia jasho lako mgawane 50/50 ingali yeye hana mchango wowote zaidi ya kuzaa watoto ambao huenda hata sio wa kwako.

Siku hizi nimekua mvivu sana kuchangia ila kuna uzi ulikuwepo humu tulichambua aina za wanawake wa kujenga nao familia na namna ya kuishi na wanawake wanaofanya kazi. Nikiuona ntautag hapa ila kwa sasa pambana na hali yako.
 
Utakuwa umesaidia sana mkuu!! Vijana wanateseka sana
 
Hapo kwenye kipato mtamuonea tu,waajiri wanatulipa ujira kidogo sana wanawake haujawahi kutosha kuchangia nyumbani na hautokaa uje utoshe... Sema ajitahidi awahi kurudi nyumbani na weekend ashinde nyumbani
 
Vijana dhaifu na wapumbavu ndio wanategemea kipato cha mke ,mwanamke anaweza kuolewa kwa hali yoyote kwa sababu majukumu makubwa ni ya mume.

Kama ulimpenda akiwa na kazi basi usitarajie kipato kutoka kwake.
 
Wacha wee,wakaka wazuri kama nyie kumbe bado mnaexist?uwe na siku yenye Baraka kweli kweli leo
 
Sio kweli kipato cha mwanamke hakichangii....ni vile sisi hucover bills ndogo ndogo nyingi, ukizijumlisha ni nyingi ila kuangalia kimoja kimoja michosho.

mfano tu nikikaa jikoni kukarangiza, vitu vingine hamna....mara nmeagiza
peanut 6000, jam 3500 chumvi imeisha 500 hapo si nshatumia elf 10.
nmepita njiani kuna vyombo vyombo nmepitia ni pesa hiyo.

malalamiko yaelekezwe kukosekana nyumbani sio kipato. Na ukiona ni muhimu saana mpe mkeo kidaftari aweke mapato na matumizi afu uone kama hachangii
 
Haya mambo ya ndoa kuna wakati yanachosha sana na kukatisha tamaa. Na hasa mkiwa mna tofauti nyingi baina yenu ndani ya nyumba.
 
Tulieni kwanza.Ngoja niisome polepole.
Screenshot_20240412-170705_1.jpg
 
Vijana dhaifu na wapumbavu ndio wanategemea kipato cha mke ,mwanamke anaweza kuolewa kwa hali yoyote kwa sababu majukumu makubwa ni ya mume.

Kama ulimpenda akiwa na kazi basi usitarajie kipato kutoka kwake.

Hoja si kipato cha mwanamke!! Hoja kuu hapa ni "nafasi yake kama mke na mama watoto" ipo wapi??

Kama nyumbani haonekani kwa madai yupo kazini, mchango wake wa kazini kwa familia nao haupo!! Tumuweke kundi gani maana hapa hata dada wa nyumbani ni muhimu kuliko yeye!!
 
Pumbavu nyie
Mnakimbilia kuoa madem waajiriwa mkidhani ndo mtapata maendeleo upesi,
Sasa mnalia na kusaga meno
Kufeni.
 
Hoja si kipato cha mwanamke!! Hoja kuu hapa ni "nafasi yake kama mke na mama watoto" ipo wapi??

Kama nyumbani haonekani kwa madai yupo kazini, mchango wake wa kazini kwa familia nao haupo!! Tumuweke kundi gani maana hapa hata dada wa nyumbani ni muhimu kuliko yeye!!
Si ulimkuta na kazi yake? Visa kama hivi ni dhaifu baada ya kumchoka mtoto wa watu ,tafuta sababu nyingine.
 
Back
Top Bottom