Matajiri wakubwa Tanzania si wafanya biashara bali ni wanasiasa, viongozi wa serikali na ndugu zao, kuonyesha kwamba kuna kitu hakipo sawa

Mkuu, utajiri sio kuangalia source,
Kina Abood walimeza viwanda vingap leo iko wapi, baba na babu zetu walikuwa wapi wakati hao wanameza viwanda,

Hayo yote ndio yanayotutofautisha, hakuna utajiri wa bahati, ni kutumia fursa zilizo mbele yetu, wazee wetu nao walikuwepo kipindi hicho cha ubinafsishaji, je walifanya nini? Kama hawakufanya kitu bas they don't deserve wealth, hizo sera mbovu zipo kwa wote, wazungu na sisi, tupambane tuache sababu nyingi, hakuna nchi perfect, hakuna nchi isio na maskini, kikubwa kwenye mazingira haya haya jua unachomokaje na unapataje pesa nying
Utapambania wapi bro bila fair play .sasa hivi kuna Ka kikundi kanadhani ndo Kako na mandate ya kuongoza.
 
matajiri wa kisiasa uongozi wanalinda sana himaya yao, mara nyingi kwa kutumia vyombo vya dola kama polisi, na sasa hata wanajaribu kutumia jeshi la ulinzi, JW.
Sasa naelewa kwa nini ma askari huitwa MBWA WA CCM.

Shida sio hao wanasiasa shida ni wananchi na majeshi yao kukubali kuwa wajinga.

Waacheni wanasiasa wale mema ya nchi.
 
Sasa naelewa kwa nini ma askari huitwa MBWA WA CCM.

Shida sio hao wanasiasa shida ni wananchi na majeshi yao kukubali kuwa wajinga.

Waacheni wanasiasa wale mema ya nchi.
Huwa nawaangalia askari wetu naishia kuwaonea huruma tu. Puppets per ce wa viongozi. Kujipendekeza 99%
 
Wataje hao wanasiasa wenye hela kumzidi Bakhresa, Mount Meru, Mo au Lake group,

Sometimes tusidanganyane sana, wanasiasa wana hela ila usiseme ndio wenye hela nying nchini, matajiri hii nchi ni wahindi na waarabu
Watanzania wengi sana wana tatizo la kutoelewa uhalisi kama wewe.

Kuna vijana nawafamu, wao kushika bilioni na kuimaliza ndani ya wiki si mchezo. Hela yao inakuja kutokana na kigogo wa juu serikalini. Anawapa deal za ku supply. Tena basi, wala sio ndugu wa karibu. Huyu kigogo ni kama yuko katika mission ya kusaidia ndugu zake wote wa karibu na mbali katika hiki kipindi ili wawe matajiri.
 
Wataje hao wanasiasa wenye hela kumzidi Bakhresa, Mount Meru, Mo au Lake group,

Sometimes tusidanganyane sana, wanasiasa wana hela ila usiseme ndio wenye hela nying nchini, matajiri hii nchi ni wahindi na waarabu
Hakuna anaemgusa rostam aziz hapo hata uyo Mo ni ccm na ashawahi mpaka kuwa mbunge
 
Ni kawaida kwamba katika nchi nyingi matajiri wakubwa utakuta ni wafanya biashara, lakini sio Tanzania. Kwa sasa wanaoongoza kwa kuwa matajiri wakubwa Tanzania ni wanasiasa waliopo madarakani au waliokuwa madarakani huko nyuma. Halafu wanafuatiwa na viongozi wa serikali, pamoja na ndugu zao.

Imefikia kwamba hata ukiwa mfanya biashara, ili utajirike kwa haraka lazima uwe na connection na wanasiasa na viongozi wa serikali, kuanzia connection za ofisi ya raisi, makamu wake au mawaziri. Hata vjana wadogo kabisa wenye hizi connections sasa wanaibukia kuwa na fedha nyingi sana za kufuja na kuishi maisha ya anasa sana.

Inatokea pia kwamba kikundi hiki cha matajiri wa kisiasa uongozi wanalinda sana himaya yao, mara nyingi kwa kutumia vyombo vya dola kama polisi, na sasa hata wanajaribu kutumia jeshi la ulinzi, JW. Hawataki watu wengine wa "kawaida" wawe kama wao. Kwa hiyo wanajaribu kuendelea umiliki wa himaya zao kwa kuwekeza katika watoto wao ili kuja kuwarithisha kuwa "wenye nchi" pamoja na utajiri wao. Hii ni kutia ndani kuendelea kufanya ufisadi mkubwa ili hata vizazi vyao vya baade viendelee kuwa katika neema ya kuwa tofauti na Watanzania wa kawaida.

Wengi wasichojua ni kwamba tatizo kubwa la serikali kukataa uraia pacha sio suala la "usalama wa nchi", bali ni usalama wa hiki kikundi kuona Watanzania walioko nje wana uhuru wa mawazo na upeo wa kuona wanachokifanya. Ndio maana hawataki watu wa diaspora wapewe nafasi ya kuja kuwa tishio kwa himaya yao. Wanawaogopa sana watu wa diaspora na wanaona kuwapa uraia pacha ni kuleta hatari ya kuondolewa katika "ufalme wao". Hawa "wenye nchi" wanajua watu wa diaspora hawana "political illiteracy" ambayo wameijenga katika Watanzania wanaoishi nchini. Wanadiaspora wana macho na wanaona, na wanaogopwa.

Lakini nataka nitoe tahadhari kwa watu hawa, kwamba katika jamii yoyote ile, hali kama hii iliyopo Tanzania huwa haidumu. Kuna wakati itafikia critical point, na kutakuwa na mlipuko mkubwa ambao ni namna fulani ya mapinduzi, ili kuliondoa tabaka hili la "wenye nchi" katika hii himaya yao ambayo kwa sasa wanaifurahia sana na kujaribu kuilinda kwa kila namna. Hili ndilo lililotokea nchi kama Tunisia na Misri, na si muda mrefu litatokea Tanzania, hali ikiendelea hivi.
Bila kuwataja na raslimali wanazomiliki itakuwa blah blah.
 
Watanzania wengi sana wana tatizo la kutoelewa uhalisi kama wewe.

Kuna vijana nawafamu, wao kushika bilioni na kuimaliza ndani ya wiki si mchezo. Hela yao inakuja kutokana na kigogo wa juu serikalini. Anawapa deal za ku supply. Tena basi, wala sio ndugu wa karibu. Huyu kigogo ni kama yuko katika mission ya kusaidia ndugu zake wote wa karibu na mbali katika hiki kipindi ili wawe matajiri.
daaaaah
nipe dili mkuu
 
Mkuu, hizo ties za wafanyabiashara na wanasiasa zipo dunia nzima, ukifuatilia huko juu nimetaja mifano,
Ties za wafanya biashara na wanasiasa zinajulikana, na zinafanya wafanya biashara wawe matajiri kwa biashara halali. Hapa tunaongelea wanasiasa matajiri kupita kiasi sio kwa kuwa wanafanya biashara, kwa kuvuta hela ya serikali inayotkana na kodi za wananchi, ku-inflate manunuzi, au kufanya miradi hewa nk. Huyo aliyenunua hekalu la bilioni 25 Dubai unafikiri yeye kazipata hizo hela kwa biashara?
 
Back
Top Bottom