T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 10,759
- 35,339
Sijasema dunia ni fair play wala sijasema kudhamini kampeni alikuwa hana hela. Mbona hujajibu kwanini Rais mstaafu Obasanjo alikuja kutatua mgogoro wa kiwanda cha Dangote?Sasa mkuu mtu kudhamin kampen za uraisi unadhani alikuwa hana hela?
Halafu hio ya kudhamin vyama au kampen ipo dunia nzima, kuanzia USA hadi andora, ni kawaida, usishangae kaka, dunia sio fair play ground, lazima kuna kuviziana kwa hapa na pale,
Kwanza unalinganishaje Marekani wakati wadhamini wa Marekani ni kisheria inatambulika na mgombea anataja amepokea kiasi gani kutoka kwa nani. Wakati kwa Dangote na Obasanjo ni makubaliano binafsi sio kisheria.
Nilichosema ni kwamba biashara za Kiafrika zina mkono wa kisiasa, hapa unapinga kisha unasema Bakhresa alipewa ekari alime sukari kisa "ana uwezo". Tena mtu huyohuyo alipewa NMC miaka ya nyuma. Kampuni ya Mayanga Construction kipindi cha Magufuli ilikuwa inapewa tenda za ujenzi za fedha nyingi hadi inazidiwa, napo utasema "ina uwezo". Magufuli kafa na kampuni hatuisikii.
Kikwete alipoondoka kampuni ya Home Shopping Centre ikafunga biashara, wakati enzi za Kikwete ilikuwa inapiga hela sana. Hutaki kuelewa unakomaa wote hao wana uwezo.