Maji ya Ziwa Victoria kuwafikia Wananchi wa Jimbo la Kaliua

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,032
974
Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Mhe. Aloyce Andrew Kwezi amesema kwamba neema ya Maji kutoka Ziwa Victoria sasa imewafikia wananchi wa Jimbo la Kaliua kwani Kampuni ya Megha Construction and Infrastructure Limited imeshafika Kaliua kuanza utekelezaji wa mradi​

Mhe. Aloyce Kwezi amesema Kampuni ya Megha Construction and Infrastructure Ltd leo tarehe 10 Julai, 2023 imewasili Kaliua kwaajili ya kuanza kutekeleza ujenzi wa mradi wa Maji ya Ziwa Victoria na usambazaji wake utanufaisha Kata mbalimbali zikiwemo Usimba, Kazaroho, Igwisi, Kamsekwa, Kaliua, Ugunga, Ufukutwa na ushokora.

Wakurugenzi wa Kampuni ya Megha Construction and Infrastructure limited wamewasili katika Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la kaliua na kuanza kupita katika Vijiji vyote ambavyo vitanufaika na mradi huo.

Mhe. Aloyce Kwezi amemshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Kuthamini wananchi wa Jimbo la kaliua ili kuwatua kina mama ndoo kichwani.

Pia, Mheshimiwa Mbunge Aloyce Andrew Kwezi amemshukuru Waziri Wa Maji, Mhe. Juma Aweso kwa uchapakazi wake na kuendeleza kazi nzuri za Kusimamia sekta ya Maji.

WhatsApp Image 2023-07-11 at 14.36.45.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-11 at 14.36.46.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-11 at 14.36.46(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-11 at 14.36.47.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-11 at 14.36.48.jpeg
 
Back
Top Bottom